"Itakuwa vyema Asia kupata ndugu" Vera Sidika afichua anapanga kupata mtoto wa pili mwaka huu

Muhtasari

•Mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 32 alisema  kwamba anaridhia sana hali yake mpya ya kuwa mama.

•Vera pia amekiri anajivunia sana maamuzi yake ya kupata mtoto kupitia njia ya upasuaji huku akieleza hakuhisi uchungu wowote na alipona haraka sana.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti na mfanyibiashara mashuhuri Vera Sidika amefichua kwamba tayari anapanga ana kupata mtoto mwingine hivi karibuni.

Alipokuwa anashirikisha mashabiki wake katika kipindi cha maswali na majibu mtandaoni Instagram, Vera alisema itakuwa vyema bintiye kupata ndugu ifikiapo mwisho wa mwaka huu wa 2022.

"Lmaoooo, nadhani baba anapanga hii kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Hata hivyo, Ndiyo. Ingependeza kwa Asia kuwa na ndugu. Labda mwisho wa 2022. Inshallah" Vera alijibu shabiki aliyetaka kufahamu iwapo kuna mpango wa kupanua familia yake.

Mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 32 alisema  kwamba anaridhia sana hali yake mpya ya kuwa mama.

Amesema alipofanya maamuzi ya kupata mtoto wake wa kwanza mwaka uliopita alikuwa amejipanga na kujitayarisha kwa hali aliyokuwa anakusudia kujiweka.

"Jambo bora zaidi ambalo nimepata hadi sasa. Huwa najiuliza kwanini sikufanya hivi mapema. Lakini najikumbusha kwamba hapo awali haukuwa wakati mzuri zaidi. Nilikuwa tayari kabisa kwa hili wakati nilikuwa tayari kwa watoto" Vera alisema.

Vera pia amekiri anajivunia sana maamuzi yake ya kupata mtoto kupitia njia ya upasuaji. Amesema hakuhisi uchungu wowote na kufichua alipona haraka sana.

"Kuchagua CS ulikuwa uamuzi bora zaidi ambao nimewahi kufanya!! Kusema kweli, upasuaji uliendelea vizuri na hata baadae. Nimepona haraka!! Nimekuwa nikifanya kazi tangu wiki ya kwanza. Kwa kweli siku hiyo hiyo baada ya upasuaji niliweza kutembea hadi bafuni peke yangu bila usaidizi" Alisema.

Mwanasoshalaiti huyo na mpenzi wake  mwanamuziki Brown Mauzo walibarikiwa na mtoto wo wa kwanza mnamo Oktoba 20 mwaka jana.