Khadija Kopa akana kukosana na Mama Diamond Platnumz

Muhtasari

•Khadija Kopa amekuwa akizungumziwa sana katika mitandao ya kijamii  kwa madai ya uhusiano wa Bintiye Zuchu na  Diamond Platnumz.

•Kulingana na mitandao ya Bongo kuna tetesi kwamba Mama Dangote hakufurahishwa na habari za wawili hao kuhusishwa kimapenzi.

• Kopa alisema...Sijawahi kuwa na namba yake ila kama kuna kitu cha dharura , nitaipata na kumpigia.

 

Khadija Kopa
Khadija Kopa
Image: Hisani

Baada ya madai kuwa Diamond anauhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki wa  lebo yake Wasafi, Zuchu, kumeibuka tetesi kwamba urafiki baina ya Mama wa Diamond na mamake Zuchu umesambaratika.

Khadija Kopa amekuwa akizungumziwa sana katika mitandao ya kijamii  kwa madai ya uhusiano wa Bintiye Zuchu na  Diamond Platnumz.

Tuhuma hizo  ambazo hazijathibitishwa na  mastaa hao , Diamond na Zuchu  zimekuwa zikienezwa  kwa nitandao ya kijamii.

Kulingana na mitandao ya Bongo kuna tetesi kwamba Mama Dangote hakufurahishwa na habari za wawili hao kuhusishwa kimapenzi.

Khadija Kopa akizungumza kuhusu madai hayo ameeleza kwamba yeye na Mama Dangote hawaja kosana na kusema hana nambari yake simu ila wakikutana uongeo kama marafiki.

Sisi ni marafiki na tunakata na kucheka, hatujawai kutofautiana. Kwa hivyo, acha kuunda vyama sisi ni watu wa kawaida ambao watoto wetu wametuleta pamoja tangu waanze kufanya kazi pamoja,"alisema Khadija Kopa

Kutokana na kauli yake ya kuwa wao ni marafiki aliombwa kumpigia Mama wa Diamond simu ambapo alikataa kwa kusema hana muhimu la kumwambia.  

Sijawahi kuwa na namba yake ila kama kuna kitu cha dharura , nitaipata na kumpigia. Muda mwingi nikitembelea duka la Esma namkuta yupo na tunaongea. Kujenga chuki miongoni mwetu ni kinyume cha Mungu. alidokeza