'Hamjaniajiri!' Jaguar awambia wasanii wanaomuomba msaada

Muhtasari

• Jaguar amewataka wasanii ambao wanahulka ya kuomba msaada wakati mambo yanapowaendea mrama kukoma.

• Alisema wasanii wengi wamekuwa wakimpigia simu kutaka msaada  na kinachomshangaza zaidi ni kuwa kuna baadhi ya wasanii hawachukulii muziki kama biashara.

• Mimi ni msanii lakini sikwenda kuomba kura nikiwa mwanamuziki, sikuchaguliwa na wanamuziki wala si mwakilishi wao bungeni.

 

JaguarJ.000
JaguarJ.000
Image: Hisani

Mwanamuziki na mbunge Charles Njagua Kanyi, maarufu Jaguar amewambia wasanii ambao wanahulka ya kuomba msaada wakati mambo yanapowaendea mrama kukoma.

Akizungumza kwenye redio moja nchini mhunge huyo aliwataka wasanii washughulike na kazi zao za  muziki kwani si wao walimchagua ni wakazi wa Starehe ndio walimpa mamlaka ya kuwaongoza.

“Mimi ni msanii lakini sikwenda kuomba kura nikiwa mwanamuziki, sikuchaguliwa na wanamuziki wala si mwakilishi wao bungeni.Nilipigiwa kura na watu wa Starehe na ni watu ninaowawakilisha. Kuna ahadi niliyowapa watu wa Starehe na sina budi kuitimiza." Jaguar alisema.

Alisema wasanii wengi wamekuwa wakimpigia simu kutaka msaada  na kinachomshangaza zaidi ni kuwa kuna baadhi ya wasanii hawachukulii muziki kama biashara jambo ambalo linawafanya washindwe kujituma kwenye tasnia ya muziki.

"Sijui wasanii walipata wapi mawazo ya kusaidiwa. Wengine hawachukulii muziki kama biashara, hawajui hata wanachotakiwa kufanya. Wanatumia pesa zao vibaya na wanapofanya fujo wanaanza kusema Jaguar hawasaidii wasanii." alidokeza 

Isitoshe aliwahimiza  wanamuziki kuwekeza na fedha ambazo wanapata kwenye muziki kwa sababu muziki unabadilika kila uchao.

“Nataka kuwaambia hivi, nilikuwa natengeneza zaidi ya milioni moja na najua kuna wasanii nilikuwa nao walikuwa wanatengeneza zaidi ya milioni moja,"