Muigizaji Dorea Chege kuwania kiti cha mwakilishi wa kike,Nairobi

Muhtasari

•Maggie amekuwa wa hivi majuzi kutangaza kuwa  atakuwa kwenye kinyanganyiro cha mwakilishi wa kike kaunti ya Nairobi.

• Maggie anajulikana zaidi  kwenye kipindi cha runinga 'Maria' ambacho kilikuwa peperushwa na runinga ya citizen mwaka jana.

 

Dorea Chege
Dorea Chege
Image: Hisani

 Muigizaji nchini  Kenya Dorea Chege, almaarufu  Maggie amekuwa wa hivi punde kutangaza kwamba  atakuwa kwenye kinyanganyiro cha mwakilishi wa kike kaunti ya Nairobi.

Maggie anajulikana zaidi  kwenye kipindi cha runinga 'Maria' ambacho kilikuwa peperushwa na runinga ya citizen mwaka jana.

Kupitia ukurusa wake wa Instagram ameeleza kwamba atakuwa anagombea  kiti cha mwakilishi wa kike Kaunti ya Nairobi akiwa mgombea huru.

Dorea amejiunga na wasanii mbali mbali ambao wametangaza rasmi kuwa watakuwa debeni Agosti mwaka  huu liwe liwalo.

Baadhi ya watu mashuhuri nchini Kenya ambao wametangaza wazi kuwa watakuwa debeni ni ikiwemo Jalang'o, Mc Jessyi, Rufftone  na Prenzo.