Khadija Kopa amwandikia Zuchu ujumbe wa kipekee afichua tarehe ya harusi yake

Muhtasari
  • Khadija Kopa amwandikia Zuchu ujumbe wa kipekee afichua tarehe ya harusi yake
Khadija Kopa, Zuchu
Khadija Kopa, Zuchu
Image: HISANI

Ni furaha ya kila mama kumuona msichana wake au mwanawe akifunga pingu za maisha na mpenzi wake.

Msanii wa bongo Zuchu na Diamond Platnumz walivuma sana wiki jana baada ya uhusiano wao kufichuliwa.

Mashabiki na wanamitandao walikejeli uhusiano wao, huku baadhi yao wakimuonya Zuchu.

Khadija Kopa mama yake Zuchu kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook amemwandikia Zuchu, ujumbe wa kipekee huku akifichua tarehe ya harusi yake.

"Zuhura mwanangu Nimekulea kwenye maadili na Najua wewe ni binti mwenye maamuzi sahihi na mimi kama Mama yako niseme sina budi kukusapoti .

Tarehe 14 inaenda kua siku yako kubwa hakuna mwanamke asie na ndoto hii.M/Mungu akakusimamie najua hutoniangusha .

siku hii isiwe tu siku yako kubwa duniani basi pia ikawe ndo mwanzo wa maisha mapya yenye Furaha .M/Mungu Akulinde kiziwanda changu Amin," Aliandika Khadija.

Kulingana na asilimia kubwa ya mashabiki ii ndio siku ambayo Zuchu na mpenzi wake watafunga pingu za maisha.

Baada ya madai hayo Zuchu hajajitokeza wazi wazi kukana au kubali madai hayo, ilhai mama yak alidai kwamba hana shida yeyotee iwapo mwanawe anampenda Diamond Platnumz.