Mzae kamtoto kazuri na mkaite Romeo! Romy Jons amwambia Diamond

Muhtasari

• Mcheza Santuri wa msanii Diamond, Romy Jons ameweka mkanda wa video kwenye ukurasa wake wa Instagram, video hiyo ikionesha Diamond na Zuchu wakiwa wameandamana katika hafla moja ya harusi kwenye sehemu ambayo Jons ameitaja kuwa Madale na amemshauri Platnumz kutulia na kuzaa mtoto na kumuita Romeo.

Diamond Platnumz na Zuchu
Diamond Platnumz na Zuchu
Image: INSTAGRAM

Kufikia sasa kila mtu na haswa watumizi wa mitandao ya kijamii wamejua bayana kwamba msanii nguli wa bongofleva, Diamond Platnumz ana mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenza kwenye rekodi lebo ya Wasafi, Zuchu

Minong’ono ya chini kwa chini imekuwa ikizagaa mitandaoni kuhusu uwezekano wa wawili hao kuwa wapenzi kwa muda mrefu lakini wiki jana ilibainika ni kweli mara baada ya mwanahabari Juma Lokole kusema kwamba Diamond na Zuchu ni wapenzi.

Taarifa hizo zilifuatiziwa na mamake msanii Zuchu kuonekana kulifurahia jambo hilo huku kukitokea taarifa kinzani kutoka kwa mamake na Diamond, ambaye alionekana kupinga ndoa ya Diamond na Zuchu ambayo inatarajiwa kufanyika siku ya wapendanao Februari 14

Mcheza Santuri wa msanii Diamond, Romy Jons ameweka mkanda wa video kwenye ukurasa wake wa Instagram, video hiyo ikionesha Diamond na Zuchu wakiwa wameandamana katika hafla moja ya harusi kwenye sehemu ambayo Jons ameitaja kuwa Madale.

Romy Jons
Image: Instagram

Katika video hiyo,mcheza santuri Romy Jons amempa wosia msanii Diamond, “MDOGO ANGU NASIBU UKATULIE SASA. MZAE NA KATOTO KAZUUURI MKAITE ROMEO”