Jamani! Kumbe wallpaper ya Zuchu ni picha Diamond

Muhtasari

•Habari za  Zuchu kutoka kimapenzi na bosi wake, Diamond  Platnumz zimekuwa kwenye mitandao wa kijamii kwa takribani mwezi tatu.

•Zuchu kwenye mahojiano  yaliyofanyika Jumatano nchini Tanzania ilibainika picha ambayo ameweka kwenye wallpaper yake si yake ila ya bosi wake Diamond Platinumz.

Diamond Platnumz na Zuchu
Diamond Platnumz na Zuchu
Image: HISANI

Kama ilivyoada penye moshi hapakosi moto, tetesi na uvumi  za mahusiano baina ya Zuchu na Diamond platinumz zimeonekana kuendelea kuwa ngumzo mitandaoni kila uchao.

Habari za  Zuchu kutoka kimapenzi na bosi wake, Diamond  Platnumz zimekuwa kwenye mitandao ya kijamii kwa takribani miezi mitatu.

Zuchu kwenye mahojiano  yaliyofanyika Jumatano nchini Tanzania ilibainika picha ambayo ameweka kwenye wallpaper yake si yake ila ya bosi wake, Diamond Platinumz.

Isitoshe,alipofika kwenye kituo  hicho cha habari alipokuwa akihojiwa alieleza wazi  kuwa Diamond alimpigia simu kuhakikisha kama aliwasili kwenye mahojiano kwa wakati.

Ingawa Zuchu alionekana kukana madai kwamba wanachumbiana na bosi wake, alifichua kuwa siku ya wapendanao atawambia mashabiki wake ukweli kuhusu mahusiano yake.

Ikumbukwe Jumatatu Mamake Zuchu, Khadija Kopa aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram akimtakia mwanawe ndoa ya furaha huku akieleza hana shaka na maamuzi ya mwanawe.

Zuchu anakaribia kufikisha miaka miwili kwenye lebo ya Wasafi, ambapo ameonekana kupata wafuasi wengi, si kwa mitandao ya kijamii bali pia kwenye youtube.