Jux akerwa na kitendo cha Harmonize Kulikoni?

Muhtasari

• Ameeleza wazi kuwa alikerwa na kitendo cha Harmonize kumhusisha kwenye orodha ya wasanii ambao wanatarajia kutumbuiza kwenye tamasha hio.

• Miongoni mwa wasanii ambao walikuwa kwenye orodha ni ; Kusah, Jux, Eddy Kenzo, Ibra  na Otile Brown

 

Juma Jux
Juma Jux

Msanii wa Tanzania Juma Mussa almaarufu Jux ameeleza wazi kuwa alikerwa  na kitendo cha Harmonize cha kupanga tamasha kisha kuchapisha jina lake  kwenye orodha ya majina ya wanaotarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo bila idhini yake.

Kupitia kituo kimoja cha Burudani nchini  humo, Jux ameeleza kuwa hakuna habari ambazo alipewa na Harmonize kuwa kwenye hafla anayoandaa hivi karibuni.

Harmonize Jumatatu aliweka baadhi ya wasanii ambao alikuwa anatarajia kutumbuiza mashabiki wake miongoni mwa wasanii hao alikuwepo Jux.

Mara ya kwanza kuongea naye alinieleza kuhusu hiyo show,nikamwambia nisawa kisha nikampa namba ya meneja wangu ili waweze kukubaliana, nilishangazwa kuwa jina langu lilikuwa kwenye orodha ya wasanii ambao watakuwa kwenye show yake,"alisema Jux  

Miongoni mwa wasanii ambao walikuwa kwenye orodha ni ; Kusah, Jux, Eddy Kenzo, Ibra  na Otile Brown. Juma Jux alikiri kuwa hakuwa na mwaliko rasmi kwenye show hiyo na haoni kama atahudhuria.