Mwijaku amshauri harmonize baada ya wandani wake kumsaliti

Muhtasari

• Mwandani wa Harmonize, Mwijaku ameshauri Mwimbaji Harmonize kutokata tamaa kipindi hiki ambacho wandani wake wanamsaliti huku akieleza anayepaswa kudunisha mtu ni Mungu pekee

• Wanadamu tunakuwa wepesi kusahau na kuhukumu kuliko Mungu,lakini maandiko yametupa nuru na hekima ya kuacha kazi ya kumshushaa mtu 

Mwijaku
Mwijaku
Image: instgram/mwijaku

Mwandani wa Harmonize, Mwijaku amemshauri Mwimbaji Harmonize kutokata tamaa kipindi hiki ambacho wandani wake wanamsaliti huku akieleza anayepaswa kudunisha mtu ni Mungu pekee.

Kupitia ukurusa wa instagram,Mwijaku ametoa taarifa refu huku akieleza wanadamu wameumbwa na tabia za kusaliti na kukosoa watu kwa kazi zao wanazofanya.

Hivi Majuzi urafiki baina ya H-Baba ulionekana kuzorota wakati H-Baba ali-unfollow Harmonize kitu ambacho kilichukuliwa  kuwa urafiki baina yao umefika ukingoni.

“Wanadamu tunakuwa wepesi kusahau na kuhukumu kuliko Mungu, lakini maandiko yametupa nuru na hekima ya kuacha kazi ya kumshusha mtu au kusema wanadamu sababu Mungu pekee ndio huinua na kuwashusha wanadamu. Na si sababu ya Chawa mmoja wa kisukuma,”

Hii imewadia baada mwandani wa Harmonize kuonekana akisifia kazi za Diamond  Platnumz kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Akizungumza kuhusu mamuuzi ya H-baba kuonekana akisifia mwimbaji nguli wa Tanzania alieleza kwamba yeye hana sababu za kutoa kasoro maamuzi ya H-Baba ila akumbuke mazuri aliyotendewa wakati alikuwa  na urafiki na Harmonize.

“Sina haki na mamlaka ya kumtoa kasoro H-Baba  juu ya Harmonize, sababu najua madhara waliyopata marafiki wa Nabii Ayubu, kipindi cha majaribu yake,” alieleza.