Staa wa Bongo, Q-Chillah afunguka kuhusu kilichopelekea kuvunjika kwa ndoa zake mbili

Muhtasari

• Q-Chillah alifichua kwamba kwa sasa hana mchumba baada ya mahusiano yake ya hapo awali kukosa kufua dafu.

•Alifichua kwamba ukosefu wa fedha za kutosha ulifanya ashindwe kugharamia mahitaji ya mpenzi wake wa pili

Qchillah
Qchillah
Image: HISANI

Mwanamuziki tajika kutoka bongo Aboubakary Shaaban Katwila almaarufu kama Q-Chillah amefunguka kuhusu ndoa zake mbili ambazo zilisambaratika.

Akiwa kwenye mahojiano na Wasafi Media, Q-Chillah alifichua kwamba kwa sasa hana mchumba baada ya mahusiano yake ya hapo awali kukosa kufua dafu.

Kigogo huyo wa muziki ambaye amekuwa akitumbuiza kwa miaka mingi alieleza kwamba ndoa zake mbili zilivunjika katika mazingira tatanishi na kuathiri maisha yake.

"Ndoa yangu ya kwanza nilikuwa na mwanadada aliyeitwa Tabata.Ilikuwa ya siri. Ilivunjika katika mazingira ambayo nilijiuliza maswali mengi sana.Ilibidi nianza kusuali, nilijiuliza imefanyika vipi? Nilijiuliza imetendeka vipi?" Q Chillah alisema.

Mwanamuziki huyo alisema kwamba mke wake wa pili alikuwa mtu maalum sana katika maisha yake.

"Alikuwa mwanamke mrembo. Alikuwa na udhubutu. Kwangu yeye ni shujaa. Kwa sasa tumetengana lakini" Alisema.

Q Chillah alisema hali ya kutoelewana ilichangia ndoa yake na mwanadada huyo kuvunjika licha ya upendo mkubwa ambao ulikuwa kati yao.

Alifichua kwamba ukosefu wa fedha za kutosha ulifanya ashindwe kugharamia mahitaji ya mpenzi wake wa pili.

"Watoto wazuri wanahitaji vitu vingi.Yeye ni mrembo. Alitaka kuwa na nywele nzuri. Alitaka kuwa na mapambo na nguo nzuri. Sikuwa nafanya shoo. Nilitaka kumtunza kama mke sio kama mbwa. Nilitaka kumtunza ilivyofaa" Alisema.

Mwanamuziki huyo alifichua kwamba ilifika hatua ambapo mkewe akawa amechoka na akaamua kuondoka.