Serikali ya Tanzania kugharamia matibabu ya Profesa Jay

Muhtasari

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alitangaza kuwa serikali yake itagharamia matibabu ya mwanamuziki huyu sifika.

Mwanamuziki Joseph Haule almaarufu kama Profesa Jay
Mwanamuziki Joseph Haule almaarufu kama Profesa Jay
Image: HISANI

Mwanamuziki  na mwanasiasa mashuhuri kutoka Tanzania Joseph Haule almaarufu Profesa Jay amekuwa hospitalini kwa kipindi cha takriban wiki nne akiwa katika hali mahututi.

Siku ya Jumamosi rais Samia Suluhu Hassan alitangaza kuwa serikali yake itagharamia gharama ya  matibabu ya mwanamuziki huyu sifika ambayo imeendelea kupanda kila siku.

Haya yanajiri baada ya kufichuliwa kwamba  afya ya msanii huyo sio shwari na familia yake kwa ushirikiano na baadhi ya watu mashuhuri kupanga jinsi ya kuomba michango ya kufanikisha matubabu yake.

Jumamosi iliyopita familia ya Profesa Jay ikishirikiana na kituo kimoja cha habari nchini humo waliandalia mbunge huyo wa zamani wa Mikumi hafla maalum ya  maombi.

Maombi hayo yalihudhuriwa na watu  wa tabaka mbalimbali na kwa pamoja wakamtakia mwamuziki huyo afueni ya haraka.

Habari za kuugua kwa Profesa Jay  zilisambaa  mitandaoni  wiki jana na maelfu ya wanamitandao wamekuwa wakimwandika jumbe za  afueni ya haraka.