Alex Mathenge azua shaka kuhusu zawadi za Bahati na Diana

Muhtasari

• Mcheshi Alex Mathenge ameibua mashaka kuhusu zawadi ambazo msanii Bahati na mpenziwe Diana Marua wamekuwa wakipokezana

• Mathenge anahoji kama zawadi hizo ni kweli basi Diana Marua kufikia sasa angekuwa na magari zaidi ya saba

Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Mcheshi Alex Mathenge ameibua mashaka kuhusu zawadi ambazo msanii Bahati na mpenziwe Diana Marua wamekuwa wakipokezana tangia mahusiano yao kushika kasi.

Akiandika katika instastories zake, Mathenge ametilia shaka zawadi wawili hao hupokezana mara kwa mara na kusema kwamba huenda zikawa ni zawadi hewa na ni njia moja ya kutafuta kiki mitandaoni.

Mathenge anahoji kama ni kweli basi Diana Marua kufikia sasa angekuwa na magari zaidi ya saba tangia aanze kupokezwa zawadi za magari na mpenzi wake Bahati.

Bahati na Diana Marua wamekuwa wakipokezana zawadi za magari katika kutimiza kumbukumbu mbali mbali zikiwemo zile za kusherehekea ndoa yao, kesherekehea kuzaliwa kwa mtoto, sikukuu za valentino miongoni mwa zingine.

Wikendi iliyopita, msanii Bahati alimmzawidi mpenziwe gari aina ya Landcruiser Prado TX miongoni mwa zawadi nyingine nyingi za siku kuu ya wapendanao, Valentino na hili limeibua maojni mkanganyiko mitandaoni baadhi wakidai ni vizuri wanavyozawidiana huku wengine wakisema ni kiki tu wanatafuta kwa kukodisha magari kutoka kwa minada na kisha baadae kuyarudisha.

Zawadi hizi ambazo Diana Marua haonekani kudumu nazo mara baada ya kuzionesha mitandaoni ndicho kitu kilimfanya Mathenge kutilia shaka uhalali na uhalisia wa zawadi hizi.

"Kama hizi vitu huwa kweli, Diana anafaa kuwa na gari saba by now. Hizi gari huwa zinaenda wapi?" alihoji Mathenge

Je, wewe unahisi zawadi hizi baina ya Bahati na Mkewe ni za kweli ama ni kiki tu mitandaoni, na kama ni kweli, hizo zawadi huwa zinaenda wapi baada ya kuzawidiana, ikizingatiwa kwamba hawaonekani wakizitumia katika mizunguko yao baada ya kuzawadiana?