Sikuwa najua niliachwa-Carrol Sonnie ajibu madai ya kuachwa kabla ya kujifungua mwanawe

Muhtasari
  • Carrol Sonnie ajibu madai ya kuachwa kabla ya kujifungua mwanawe
Carrol Sonnie
Image: Radiojambo

Wiki chache zilizopita mcheshi Mulamwah na mama wa mtoto wake Carrol Sonnie wamekuwa wakianikana mitandaoni, na kufichua sababu kuu ya kuachana.

Wawili hao waliachana miezi 2 baada ya kubarikiwa na kifungua mimba wao.

Carrol akiwa kwenye mahojiano na Radiojambo, alikiri kwamba amemsamehe Mulamwah kwa yote ambayo alisema, kwani anamjali mwanawe Keilah.

Huku akijibu madai ya Mulamwah kwamba waliachana akiwa na ujauzito wa miezi 3 Carrol alisema;

"Mimi sikuwa najua kwamba niliachwa nikiwa na ujauzito wa miezi 3, ukweli ni kuwa sikuona, kile najua tuliachana miezi 2 baada ya kubarikiwa na mtoto wangu," Sonnie Alisema.

Aidha Carrol alisema kwamba hakushtuka baada ya Mulamwah kuweka hadharani kwamba wameachana rasmi kwani alikuwa anamjua mpenzi wa Mulamwah.

" Wazazi wake wamekuwa wakinipigia simu na kunishika mkono, sina uhusiano mbaya nao, kwa sasa sitaki kuchumbiana nataka kujijua mwenyewe," Carrol Alizungumza.