'Nawaza' ya Diamond yashabikiwa mpaka bungeni

Muhtasari

• Spika wa bunge la Jamhuri ya Tanzania Dkt Tulia Ackson ameishabikia ngoma ya Nawaza ya Diamond Platnumz na kusema kwamba inatafakarisha sana mambo ya uhalisia.

Msanii Diamond Platnumz na spika wa bunge la jamhuri Dkt. Tulia Ackson
Msanii Diamond Platnumz na spika wa bunge la jamhuri Dkt. Tulia Ackson
Image: Facabook, Instagram

Moja ya ngoma pendwa zaidi katika albamu fupi ya FOA yake msanii Diamond Platnumz ambayo ni Nawaza imefagiliwa sana na wengi haswa kwa maudhui na ujumbe mzito ambao ngoma hiyo inasheheni.

Katika miaka ya hivi karibuni, wasanii wengi sijui waliambiwa ama wamekuwa wakijua kwamba ili kutoboa tundu katika soko la muziki ambao una upinzani wenye ncha kali, eti lazima msanii ufanye tungo za kimahaba na kimapenzi.

Ni kweli kwamba ngoma nyingi zenye maudhui ya kimapenzi zimekuwa zikifanya vizuri katika miaka ya hivi karibuni, na haswa kutoka kwa wasanii wengi wa miziki ya kizazi kipya Afrika Mashariki.

Ila safari hii Diamond alitoka nje kidogo na kuleta kitu kipya katika Nawaza ambapo imesemekana ameimba masuala ya kihalisia kama ambavyo aliwahi fanya katika ngoma za awali za Utanipenda na Acha Nikae Kimya.

Wimbo wa Nawaza ndio ambao umeshabikiwa mno kwa maudhui yanayomuacha kila mtu akirejea nyuma na kufanya tathmini ya kikweli kuhusu maisha na watu wanaomzunguka kwa jumla.

Sema wimbo huu haijashabikiwa na watu wa kawaida tu bali umesikilizwa hadi na Spika wa bunge la Jamhuri ya Tanzani, Dkt Tulia Ackson ambaye pia anasema goma hilo linamgusa pakubwa.

Kwenye FOA na mimi nina wimbo wangu ambao ni Nawaza. Ni wimbo unaotafakarisha juu ya mambo mbalimbali ambayo anajiuliza Diamond kama yakitokea au asipokuwepo itakuwaje?” alisema Ackson.

Wengi waliosikiliza Diamond katika goma hilo wanasema kwa asilimia kubwa anazungumzia uhalisia wa maisha yake na sababu ya matukio mbalimbali kama ugomvi kati yake na msanii mwenziwe Alikiba muongoni mwa maudhui mengine ambayo anayataja.