Diamond kumuoa mpenzi wake Jumatatu usiku? Wachache waalikwa kwenye hafla yake maalum

Muhtasari

•Hafla hiyo imehusishwa na tetesi ambazo zimekuwa zikieenea kwamba anapanga kufunga pingu za maisha na kipenzi chake kipya.

•Hivi majuzi Mama Dangote alifichua kwamba ni kweli ndoa ya mkeka ilifanyika na kutangaza mengi yangewekwa bayana Aprili 11.

Diamond Platnumz kufunga ndoa Jumatatu usiku?
Diamond Platnumz kufunga ndoa Jumatatu usiku?
Image: INSTAGRAM// MAMA DANGOTE

Ni waalikwa wachache tu watakaohudhuria shughuli maalum kwa Diamond Platnumz itakayofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Jumatatu jioni.

Jumapili, Diamond alitangaza kwamba kitakachokuwa kinaendelea usiku huo kitapeperushwa moja kwa moja kwenye runinga yake Wasafi TV kwa minajili ya wale ambao hawatahudhuria

"Najua ni wengi mnanipenda na KuniSupport kwa hali na mali... Wote mnathamani kwangu na nilitamani kufanya jambo ambalo wote tungeweza kuhudhuria, lakini kwa siku ya kesho imeniladhimu kuwaalika wachache kisha hafla ya pamoja itafuata... kwa mtaokua majumbani mtaweza kushuhudia live kupitia Wasafi TV kuanzia saa moja ya Usiku," Diamond alitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Ingawa staa huyo wa Bongo hakutangaza kitakachofanyika usiku wa Jumatatu, wengi waafla hiyo na tetesi ambazo zimekuwa zikieenea kwamba anapanga kufunga pingu za maisha na kipenzi chake kipya.

Siku za hivi majuzi Diamond ameonekana kazama ndani kabisa katika bahari la mahaba huku mama yake, Mama Dangote akiendelea kumshinikiza afunge ndoa na mpenzi wake hivi karibuni.

Hivi majuzi Mama Dangote alifichua kwamba ni kweli ndoa ya mkeka ilifanyika na kutangaza mengi yangewekwa bayana Aprili 11.

"Ni kweli kulikuwa na ndoa ya mkeka. Tutazungumza zaidi Tarehe 11 Inshallah," Alisema.

Kulikuwa na tetesi kwamba Diamond tayari alifunga ndoa na kipusa kutoka Zanzibar katika harusi iliyohudhuriwa na wachache tu.