(+video) "Ali'cheat nikampa adhabu ya kulipia upasuaji wangu wa pua"

Mwanamke huyo aisema hakuwa anataka kuhisi muda wake umeharibiwa katika mahusiano hayo

Muhtasari

• Alidokeza kwamba hata baada ya mchumba wake kulipia gharama ya upasuaji wa pua bado alichepuka tena.

Mwanamke mmoja katika mtandao wa TikTok amezua mjadala mkali mtandaoni kuhusu wapenzi wa kiume wanaochepuka nje ya mahusiano na ndoa kwa kutoa kile alichokitaja kuwa suluhu la kudumu katika suala hilo.

Kulingana na video amabyo aliipakia kwenye mtandao wa TikTok, mwanamke huyo ambaye hata akaunti yake hajaipa jina bali nambari tu anasema kwamba alimfumania mpenziwe akichepuka na mwanamke mwingine na akamkasirikia vibaya.

Mchumba huyo wake aliaibika na kumuuliza ni nini angependa kumfanyia ili hali hiyo isijirudie tena, cha kushangaza ni kwamba mwakamke huyo alimtaka mwanaume wake kumlipia gharama ghali ya kufanyiwa upasuaji wa pua kama fidia ya kuchepuka nje ya mahusiano yao.

“Wakati unamkuta akichepuka na akuulize ungependaakufanyie nini ili kurekebisha hali hiyo,” mwanamke huyo alifuatisha video hiyo kwa maneno hayo.

“Nilifanya hivi wakati nilipomkuta akichepuka, nilimwambia kwamba nitaendelea kukaa na yeye ila kwa sharti kwamba asimamie gharama ya upasuaji wa pua yangu, kitu ambacho nilikuwa nakihitaji kwa muda mrefu. Nilifanya hivi kwa sababu kuchepuka kwake kuliniletea nafsi yangu kukosa amani kabisa na pia kwa sababu sikuwa nataka muda wangu katika mahusiano hayo kuharibiwa tena juu nilifikiria itakuwaje endapo atachepuka tena,” mwanamke huyo alieleza kweney video hiyo fupi.

Mwanamke huyo alifichua kwamba mchumba wake alienda tena akachepuka na sasa kuuliza iwapo gharama hiyo aliyoipata ya upasuaji wa pua kutoka kwake ilikuwa stahiki kwa muda wake kwenye mahusiano yale na kujiridhisha kwamba ndio ilistahiki.