"Ikulu sio kanisa"- Annita Raey amchokoza rais Ruto

Annitah alisema kuwa vifo vinavyofanyika huko Turkana vinafaa kushughulikiwa ila si kuambia wananchi waombe kuhusu hali hiyo

Muhtasari

•Hii imefuatia ibada iliyoandaliwa Ikuluni Nairobi na rais William Ruto iliyohudhuriwa na viongozi wa kanisa zaidi ya 40.

Annitah Raey
Image: Caroline Mbusa

Mwanamtandao Annitah Raey atoa maoni yake kuhusu ibada iliyoandaliwa kwenye Ikulu ya Nairobi wikendi hii iliyopita.

Annitah alisema kuwa licha ya kuwa mfuasi wake Rais William Ruto, Mama wa Taifa Rachel Ruto na mume wake wamezidi kiwango chao cha mambo ya dini.

“Mimi ni mfuasi wa Ruto sana lakini yeye na bibi yake wamezidi kwa mambo ya dini,”alisema.

Annitah alisema kuwa uhusiano wetu na Mungu ni wa kibinafsi na isiwe kwamba wao ndio wapekee kwake Mungu.

Aliongeza na kusema kuwa Ikulu ya Nairobi si kanisa na wanapaswa kufungua kanisa ili kuisukuma ajenda hiyo.

“Uhusiano wetu na Mungu ni wa kibinafsi. Usifanye ikae ni kama una uhusiano wa kipekee na Mungu. Ikulu sio kanisa, fungueni kanisa ili muweze kuisukuma ajenda hiyo,” alisema.

Kwa wakati huo huo, Annitah alisema kuwa vifo vinavyofanyika huko Turkana vinafaa kushughulikiwa ila si kuambia wananchi waombe kuhusu hali hiyo.

“Watu wanakufa Turkana, shughulika na suala hilo, usituambie tuombe kuihusu,”alisema.

Hii imefuatia ibada iliyoandaliwa Ikuluni Nairobi na rais William Ruto iliyohudhuriwa na viongozi wa kanisa zaidi ya 40.

Kwenye ibada hiyo rais alikuwa amewaomba makasisi waombee vitu vitatu vinavyoendelea nchini Kenya na kusababisha kudorora kwa nchi.

Miongoni mwa mambo yanayoendelea nchini Kenya ambayo Ruto alikuwa amewaomba makasisi kuombea ni alichotaja Annita.

Ruto alikuwa amewaomba makasisi hao waombee dhidi ya roho ya migogoro inayoendelea nchini ikiwemo wizi wa ng’ombe.

Hata hivyo, rais alisema kuwa atashughulikia jambo hilo.

"Tuiombee nchi yetu ili roho ya migogoro na wizi wa ng'ombe ushindwe na tutafanya jukumu letu kama serikali kuhakikisha kuwa tunakabiliana na tishio letu na kudumisha amani nchini mwetu," Ruto alisema.

Baada ya hapo Ruto aliagiza vyombo vya usalama kukabiliana vilivyo na visa vya wizi wa Ng'ombe Turkana na Pokot baada ya maafisa 11 kupoteza maisha yao kutokana na wizi wa ng’ombe uliokuwa huko.

" Baada ya kupokea ripoti ya kina kuhusu tukio la Turkana/pokot lililosababisha maafisa 10 wa usalama/utawala kupoteza maisha, nimeagiza mashirika ya usalama kushughulikia kwa uthabiti, madhubuti na kwa uthabiti. pamoja na wanaohusika. Wizi wa ng’ombe utakoma na sio tafadhali,” alisema.

Ruto pia aliwaomba makasisi kuomba uchumi wa Taifa la Kenya unaodorora na pia vikosi vya usalama vya nchi wanapopambana na ukosefu wa usalama na kudumisha msimamo wa Kenya.