Samidoh amshambulia shabiki aliyemtaka akae na mtoto wakati Nyamu akimsikiliza Ruto bungeni

"Sijaenda leo niko kazini, wako amemaliza kufua?" Mwimbaji huyo alijibu.

Muhtasari

•Karen ambaye hivi majuzi aliteuliwa kuwa seneta alijifungua mtoto wake wa pili na Samidoh takriban miezi saba iliyopita.

•Mtumizi wa Facebook alimuuliza ikiwa anapanga kusaidia mzazi mwenzake kukaa na mwanao wakati akiwa bungeni. 

Samidoh
Image: HISANI

Mwimbaji wa nyimbo za Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh anaonekana kutofurahishwa na wanamitandao ambao hushinda wakimuuliza kuhusu hali ya baby mama wake Karen Nyamu.

Ingawa wao sio wanandoa rasmi, Samidoh na Bi Nyamu wana watoto wawili pamoja , wa kiume (Samuel Jr) na wa kike (Wairimu).

Chini ya takriban machapisho yote ya Samidoh  kwenye mitandao ya kijamii wanamitandao kadhaa hujitokeza kumuuliza kuhusu mwanasiasa huyo.

Katika chapisho lake la Alhamisi, mtumizi wa Facebook alimuuliza ikiwa anapanga kusaidia mzazi mwenzake kukaa na mwanao wakati akiwa bungeni. 

"Haiyaa hauendi bunge teba kukalisha mtoto mama akionngeleshwa na rais?" mwanamitandao mmoja aliuliza.

Samidoh ambaye alionekana kutoridhishwa na ujumbe wa shabiki huyo alijibu, "sijaenda leo niko kazini, wako amemaliza kufua?

Karen ambaye hivi majuzi aliteuliwa kuwa seneta alijifungua mtoto wake wa pili na Samidoh takriban miezi saba iliyopita.

Mnamo Februari 26, wakili na mwanasiasa huyo asiyepungukiwa na utata alipakia picha maridadi ya mikono ya mtoto na kuiambatanisha na ujumbe, "Tunakupa utukufu wote. Tunakuabudu wewe Mungu wetu."

Inaaminika kuwa Samidoh bado ndiye baba ya mtoto wa tatu wa Nyamu ingawa wawili hao hawajakuwa  katika hali ya kuelewana kwa kipindi kirefu.

Mwezi Februari alifichua kuwa jina la kitinda mimba wake ni Wairimu. Hata hivyo haijulikani kama binti huyo atatumia jina la Samidoh kuwa jina lake la tatu kama ilivyo tamaduni katika jamii yao ya Kikuyu.

Karen na Samidoh ambao walikuwa kwenye mahusiano ya siri kwa muda mrefu wana mtoto mwingine mmoja wa kiume, Sam Juniour ambaye alizaliwa mwaka wa 2020.