(+video) Baba wa mabinti! Nameless na Wahu wafichua jinsia ya mtoto wao

Wanamuziki Nameless na Wahu wamefanya sherehe ya ujauzito wa mwanao mtarajiwa ya kufichua jinsia yake.

Muhtasari

• Walifichua jinsia ya mtoto wao kwa kutoboa kibofu na pia kutumia moshi, ambavyo vyote vilionyesha rangi ya waridi.

Wahu// Nameless

Wanamuziki Nameless na Wahu wamefanya sherehe ya uja uzito wa mwanao mtarajiwa ya kufichua jinsia yake.

Sherehe hiyo ya kufana ilihudhuriwa na watu wengi wakiwemo watu maarufu na marafiki wa wapenzi hao.

Wapenzi hao wawili walifichua kuwa wanatarajia mtoto wa kike ambaye atakuwa wa tatu sasa miongoni mwa hao wengine.

Walifichua jinsia ya mtoto wao kwa kutoboa kibofu na pia kutumia moshi, ambazo zote zilionyesha rangi ya waridi.

Wote walichapisha kwenye ukurasa wa Instagram na kusema kuwa wamefurahia kugundua jinsia ya mwanao wa tatu.

Walisema kuwa wameridhika na kuwa wana furaha kuwalea watoto wasichana na kuwapa nidhamu za kimalkia.

"Nahisi kuheshimika kuwa mwenyekiti wa baba wa wasichana, tumefurahia wajibu wetu na tuko tayari," Wanandoa hao waliema.

Walitakiwa mema na mashabiki wao wakiwemo watu wengine maarufu:

@diana_marua - Hongera

@akotheekenya - Baaas hongera mpenzi.

@ruebaby - Watoto wa kike ni baraka. Hongera

@nanaowiti - Hongera

Wamefanya sherehe hiyo  baada ya kupiga picha ya uja uzito huo na kuweka mtandaoni huku wakifurahia hatua hiyo yao mpya.

Wahu na Nameless wanatarajia mtoto wao wa tatu waliofichua kua ni wa kike baada ya kuwa kwenye ndoa kwa miaka 17.