Nameless na Wahu washerehekea miaka 17 kwenye ndoa "Gazeti maarufu lilisema hawatutadumu miaka 2"

Nameless na Wahu washerehekea miaka 17 kwenye ndoa "Gazeti maarufu lilisema hawatutadumu miaka 2"

Wahu alisema kuna gazeti lilitabiri kwamab ndoa yao haingeenda zaidi ya miaka 2

Muhtasari

• “Septemba 10, 2005 nilifunga ndoa na mpenzi wangu wa miaka 8" - Wahu

Wanandoa hao wanatarajia mtoto wao wa tatu hivi karibuni
Wahu, Nameless Wanandoa hao wanatarajia mtoto wao wa tatu hivi karibuni
Image: Instagram

Mwanamuziki Wahu Kagwi na mumewe Nameless wanasherehekea miaka 17 ya kuishi katika ndoa yao.

Msanii huyo ambaye ni mjamzito kwa mtoto wa tatu alipakia video ya kitambo inayoonesha matukio jinsi yalivyokuwa wakati wa kufunga ndoa kwao miaka 17 iliyopita.

Video hiyo ilionyesha Wahu akiwasili kwenye ukumbi wa harusi kwa mashua, akiwa amevalia nguo nyeupe na ngozi ya mnyama ya kahawia.

Msanii huyo alifichua kwamab kabla ya kufunga ndoa ya Nameless mwaka 2005, walikuwa wamechumbiana kwa miaka minane. Kwa hiyo ni sahihi kusema kwamba mahusiano ya wawili hao wenye umaarufu mkubwa yamedumu kwa miaka 25.

Wahu alishangaza wengi kwa maneno ya ukakasi ambayo alifuatisha video ile nayo, kwa kusema kwamba kuna jarida moja la humu nchini lilibashiri kwamba mapenzi yao hayangezidi miaka miwili walipofunga ndoa ya kiasili mwaka 2005.

Alikashfu kampuni hiyo ya kuchapisha gazeti kwani walienda kinyume na ubashiri huo na miaka 17 baadae, bado wamegandiana pamoja kama ruba kwa mapenzi yasiyojua kufa.

“Septemba 10, 2005 nilifunga ndoa na mpenzi wangu wa miaka 8. Gazeti maarufu lilisema hatutadumu zaidi ya miaka 2....vizuri.....miaka 17 baadaye Bado tuko!! Heri njema ya miaka 17 mpenzi wangu Nameless.... Mimi ndio niko na furaha na nimebarikiwa kutembea nawe maisha haya,” Wahu aliandika.

Mahusiano ya wapenzi hawa wawili yanatumiwa kama mfano hai na watu wengi kwani wametembea safari ndefu sana katika dunia ya sasa ambayo ndoa baina ya watu mashuhuri wawili haidumu zaidi ya mwaka.

Nameless amerejea hivi majuzi kutoka ziara ya muziki Marekani alikokaa zaidi ya miezi miwili na kwa kweli wawili hao ndio utambulisho kamili kwamba ndoa si kitu cha longo longo pakiwepo wawili wanaoelewana na kupendana.