Nikama Kurogwa! Mwingizaji Omosh asema baada ya kupoteza kila kitu

Mwingizaji Omosh alisema sasa hana kitu hadi bibi yake alimwacha

Muhtasari

•Muigizaji Omosh alielezea hali yake ya sasa kuwa ya kuhuzunisha.

• Omosh pia amedokeza kuwa haishi tena na familia yake.

Omosh alia baada ya kupoteza kila kitu
Omosh alia baada ya kupoteza kila kitu
Image: instagram

Muigizaji wa zamani wa Tahidi High Joseph Kinuthia almaarufu kama Omosh ameambia mtandao wa Mpasho kwamba haendelei vizuri.

Akizungumza katika mahojiano ya hivi majuzi, Omosh alitaja hali yake ya sasa kuwa ya kuhuzunisha.

“Napitia mengi tu, sijui kama ni msongo wa mawazo au ni nini kinatokea katika maisha yangu,” alisema.

Wakati wa mahojiano, Omosh alisema alikuwa mahali fulani akijaribu kufikiria jinsi angefika nyumbani baada ya rafiki yake kumwalika kwa kazi na kukataa kumlipa.

"Kama sasa hivi, nawaza tu nitafikaje nyumbani kwangu huko Kayole. Niliwahi kuitwa kazi fulani lakini haikufanya kazi, kwa hiyo nimekwama."

Omosh pia alidokeza kuwa haishi tena na familia yake.

"Nimepoteza kila kitu katika maisha yangu, mke wangu, na kila kitu kimepotea," alisema.

Mara ya mwisho Omoshi huyo kuonekana hadharani ni alipokuwa akiombewa katika kanisa la Mchungaji Kanyari miezi michache iliyopita.

Muigizaji huyo aliyezawadiwa nyumba ambayo alisema hajahamia mahali hapo kwani watoto wake wako shuleni na hakuna shule karibu.

Nyumba hiyo  iliyoko Malaa ilikabidhiwa kwa Omosh mnamo Juni 2021 baada ya kujitokeza akidai alikuwa karibu kuondolewa kwa sababu ya changamoto ya kulipa kodi.

Image: INSTAGRAM// OMOSH KIZANGILA MWENYEWE

Muigizaji huyo amekuwa kwenye uraibu wa vileo tangu video nyingine yake akiwaomba Wakenya usaidizi kusambaa mitandaoni.

Wasiwasi ulizuka baadaye kuwa mwigizaji huyo alikuwa akipambana na  ulevi, na hivyo kutumia vibaya zaidi ya shilingi milioni moja alizopokea.

Tatizo la Joseph Kinuthia la ulevi lilianza katika Kaunti ya Nyeri, nyakati za ujana wake.

Katika mahojiano ya kina na gazeti la Mount Kenya Star, Omosh alisema alikua amezungukwa na wanafamilia ambao walikunywa vileo, na hivyo kuonjeshwa mapema.

"Nikiwa bado kijana katika Kaunti ya Nyeri, tayari nilikuwa nikijaribu kunywa pombe kutokana na shinikizo la rika na kwamba nilikulia katika jamii ambayo watu wengi wakiwemo jamaa zangu walikunywa vileo mbalimbali ikiwemo pombe. Hii ilinifanya kutaka kujaribu, " Omosh alisema.

Tabia hiyo ilizidi kuwa mbaya Omosh alipohamia Nairobi, ambapo pesa na umaarufu vilizidisha hali hiyo ya pombe.

"Kama mwigizaji wa Tahidi High, nilikuwa nikinywa bia 10 kila siku bila kujisikia chochote. Nikiwa mtu maarufu mara nyingi nilikuwa naenda kwenye tafrija, sherehe au vilabu baada ya kualikwa na marafiki au mashirika mbalimbali yaliyotoa vinywaji bure," alisema.