Mimi na wewe tumepitia changamoto - Diana Marua amwandikia mwanawe mtarajiwa ujumbe

Marua anatarijiwa kutangaza jinsia ya mwanawe mtarajiwa leo Jumanne

Muhtasari

• Mke huyo wa Bahati alisema kuwa ingawa safari hii imekuwa ndefu yenye vikwazo, bado anampenda mwanawe.

• Marua alisema kuwa mshikamano katika yake na mwanawe ni jambo muhimu katika maisha yake.

Diana Marua

Mke wa mwanamuziki Kevin Kioko almaarufu Bahati, Diana Marua alimwandikia mwanawe anayemtarajia ujumbe wa kihisia.

Ujumbe huo alioandika Marua ni ujumbe uliowagusa wengi kwa alivyoonekana kumsubiria mwanawe kwa hamu na ghamu.

Marua alisema kuwa amemtarajia mwanawe na kuwa yuko tayari kumpokea kwa mikono miwili kwa jinsi anavyompenda.

Aliongeza na kuushukuru mwili wake kwa kumsitiri mwanawe na kuwa nyumba yake kwa miezi tisa aliyokuwa mja mzito.

"Moyo wangu unadunda sana, mtoto wangu anageuka sana, nina wasiwasi mno. Siwezi ngoja kukutana nawe, upendo wangu kwako umekuwa ukikua kila siku na nimekupenda na kila kitu changu," Marua alimwandikia mwanawe mtarajiwa.

Marua aliendeleza hisia zake kwa mwanawe huku akikumbuka alichopitia miezi tisa ya kubeba uja uzito huo.

Alisema kuwa baadaye au bada ya miaka michache atamsimulia mtoto wake kuhusu upendo wake kwake na jinsi safari yao ilivyokuwa.

Alisema kuwa licha ya changamoto za safari hii ya uja uzito bado alijikakamua na kuwa mwenye nguvu kwa sababu ya mwanawe.

"Siamini nitakukumbatia kwa mara ya kwanza hivi karibuni, nitahisi joto lako na mpigo wa moyo wako kifuani mwangu. Mimi na wewe tumepitia mengi, milima na mabonde. Nilipokuwa najihisi kuwa chini ulinikumbusha nijikaze kwa ajili yako," mama huyo alisema katika ukurasa wake wa Instagram.

Mama huyo wa watoto wawili alisema kuwa kumkumbatia mwanawe itamliwaza.

"Ningeandika kitabu kuhusu safari hii yetu ndefu, labda siku zijazo nitaandika. Kwa sasa, jua kuwa uko na wazazi,familia na ndugu bora kabisa duniani,"  Marua alifafanua hisia zake.

Mama huyo ametarajia kujifungua wiki hii baada ya kutangaza kuwa amekamilisha miezi tisa ya kumbeba mwanawe.