Najivunia kuwa nawe- Milly wa Jesus amsifia mumewe Kabi

Alifichua kuwa amemfahamu baba wa watoto wake tangu akiwa na umri wa miaka 20

Muhtasari

•Kabi alikuwa anasifu siku yake ya kuzaliwa huku akisimulia  hadithi zake za zamani na umbali ambao ametoka,Alifichua kuwa wakati mmoja alipambana na uraibu wa bangi

Kabi Wajesus na Milly Wajesus
Image: Milly Wajesus Instagram

Milly WaJesus anasherehekea mumewe Kabi WaJesus  anapoadhimisha siku ya kuzaliwa  Milly alishiriki picha ya mume wake na kuwaomba mashabiki wamsaidie kumtakia kila la heri.

Alifichua kuwa amemfahamu baba wa watoto wake tangu akiwa na umri wa miaka 20.

"Tuendelee kuhesabu miaka, au tuiache Unaamini nilikujua tangu nikiwa  na miaka 20? tunajivunia kuwa nawe baba wetu tunakupenda sana. Tunakuombea neema tele katika mwaka huu mpya wa maisha yako. Uvikwe kibali, kwa jina la Yesu. Huu utakuwa mwaka wako bora zaidi ".alisema milly Milly wa Jesus.

Kabi kwa upande mwingine alishiriki na mashabiki ambao walimshuku kwa kuona mwaka mwingine. "Ni siku yangu ya kuzaliwa ya" thelathini na kitu" leo, lakini mke wangu  millywajesus anasisitiza lazima awe kwenye picha hiyo kwa sababu tunasherehekea pamoja kwa sababu tunapendana sana ...alisema.

 Kabi alikuwa amehesabu siku yake ya kuzaliwa, alishiriki hadithi zake za zamani na umbali ambao ametoka,Alifichua kuwa wakati mmoja alipambana na uraibu wa bangi.

"Kisha, Septemba 15, 2013, nilipata wokovu na kuzaliwa mara ya pili. Kwa kuogopa kurudia alisema Kabi.

"Lakini kwa mshangao, nilipomkubali Yesu kuwa mwokozi wangu, hamu ilitoweka "Lakini pia nilifanya jambo lingine muhimu nashukuru mungu ". alisema

'Sitakuvuta au sitakunywa tena, sasa Nimezaliwa tena!' Ninaamini katika uwezo wa kushuhudia imani yako, si kwa wengine tu, bali kwa mapambano yako pia." Kabi alisema.