Familia ya Wajesus yatishia kuwachulia hatua za kisheria watu waoharibu jina lao

Youtuber huyo akizungumza katika ukurasa wake wa Youtube alisema watu wanaojaribu kuongea vibaya kumhusu na familia yake wataona kilicho mtoa kanga manyoya.

Muhtasari

• Mwanablogu huyo aliongeza kuwa watu mitandaoni wamekuwa wakitumia jina lao vibaya ili waweze kupata umaarufu na kuwa sasa muda wao umefika wa kujibu mashtaka.

Image: INSTAGRAM// MILLY WAJESUS

Peter Kabi almaarufu Kabi wa Jesus akiwa na familia yake inayofahamika kama The Wajesus Family wametishia kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaoharibu jina la familia hiyo.

Youtuber huyo akizungumza katika ukurasa wake wa Youtube alisema watu wanaojaribu kuongea vibaya kumhusu na familia yake wataona kilicho mtoa kanga manyoya.

"Huto tuyoutuber channels mnajaribu kuongea vibaya, shame on you. Guyz tunawakujia na hatutawabembeleza. This time tutachukua hatua za kisheria kwa sababu tumenyamaza sana na mnafikiria sisi ni waoga" alizungumza kwa hasira.

Mwanablogu huyo aliongeza kuwa watu mitandaoni wamekuwa wakitumia jina lao vibaya ili waweze kupata umarufu na kuwa sasa muda wao umefika wa kujibu mashtaka.

Youtuber huyo wenye umri wa miaka 33 aliwakosoa watu wanaokejeli mama mkwe wake, mma ya Milly Wa Jesus, mitandaoni kutokana na muenekano wake.

Baba huyo wa watoto wawili aliongeza kuwa imewachukua muda mwingi kulitegeneza na kulifikisha jina la familia yakekupata umaarufu na hawatakubali watu kuiharibu kwa urahisi.

Mwezi Mei alipakia video kwenye akaunti yake ya Twitter akipiga densi na mama mkwe wake, Mrs Ng'ang'a, Kile ambacho Wakenya wengi walihisi ni ukaribu wa sana na mama mkwe.

Baadhi ya wafuasi wengi walijitokeza na kumshutumu vikali kwa kufanya video akionekana akimshika mama mkwe wake kwa njia ambayo mashabiki hao walihisi ilikuwa ikikiuka utamaduni wa Kiafrika.

Kabi wa Jesus alivunja kimya chake kutoka kwa kutorithika kwa wafuasi wake na kjigamba kuwa hakuna maoni ya yeyote yanayoweza kuathiri uhusiano wake na mama mkwe wake.

Aliongeza kuwa ataendelea kufanya vido hizo na Bi. Ng'ang'a licha ya hisia hasi kutoka kwa mshabiki wake.

"Bi. Nganga nakuja ili tufanye tiktok nyingine na tutavuma," Kabi aliongezea.