Maoni mseto jamaa akimzawadi mpenziwe maua na yoghurt kwa kuchora tattoo yake usoni (video)

“Nilidhani thamani ya tattoo ni vitu kama title deed au logbook… yoghurt na maua tena!?” mrembo mmoja aliuliza huku mwingine akiongeza, “aki huyu msichana hana maisha, unafanya haya yote kwa ajili ya yoghurt tu?”

Muhtasari

• Katika video ya kusasisha tukio hilo, mrembo huyo alipakia video akikabidhiwa zawadi ya maua na yoghurt na mpenzi wake ndani ya nyumba.

Mrembo aliyechora tatoo ya mpenziwe azawadiwa maua, yoghurt,
Mrembo aliyechora tatoo ya mpenziwe azawadiwa maua, yoghurt,
Image: Screengrab// TikTok (Lizah Njeri)

Watumizi wa mtandao wa video fupi wa TikTok wametoa maoni tofauti tofauti baada ya jamaa kumnunulia mpenzi wake zawadi ya maua na yoghurt pekee baada ya mrembo huyo kuchora tattoo ya jina lake kwenye paji la uso.

Mrembo huyo kwa jina Liza Njeri alipakia video ya awali akichorwa tattoo ya jina la mpenzi wake “Paul Kibe” kwenye paji la uso.

Katika video ya kusasisha tukio hilo, mrembo huyo alipakia video akikabidhiwa zawadi ya maua na yoghurt na mpenzi wake ndani ya nyumba.

Jamaa huyo kwa jina Paul Kibe alionekana jijini majira ya jioni akinunua maua na kusema kwamba ndicho chanzo kikubwa kilichopelekea yeye kuheshimiwa na mpenziwe kwa kuchora tattoo ya jina lake kwenye uso wake.

Akizungumza baada ya mpenziwe kumpa maua na yoghurt, mrembo huyo aliwashauri warembo wengine ikiwa wanataka kupewa zawadi kama hizo na wapenzi wao, basi wakachore tattoo za majina yao kwenye paji la nyuso zao.

“Ahsante, ndio maana niliweka number plate yako hapa kwenye uso wangu, ninaambia watu waweke number plate za wapoa wao pia kama wako na uhakika wanawapenda, kama hupendi mtu wako usiweke,” Njeri alisema.

Hata hivyo kitendo cha kuchora tattoo na pia kitendo cha mpenziwe kumzawadi kwa maua na yoghurt pekee vilionekana kuvutia maoni mengi kutoka kwa watu.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya watumizi wa mtandao huo;

“tattoo Kwa forehead na unalala chini?Babe!!!!” Rylen.

“I thought tattoo would be worth title deed or log book 🤔 yoghurt na maua tena😏😂” Annitah Lovely.

“hiyo si tattoo it's maybe a henna or something akichorwa she wasn't feeling the pain na ni kwa kichwa ..anyways ur trending,” Goodness Barbie.

“dem unachora tattoo kwa forehead na unadoz chini😂😂” It’s Wangui.

“Aki huyu hana maisha...All this for yoghurt 😂” Winnie Wangoi.

“Ata uchore tattoo Kwa kinem** bado atacheat🤣🤣🤣it can never be me” Fifi.

Tazama video hiyo hapa kisha utoe maoni yako kuhusu watu kuchora tattoo kutokana na msukumo wa mapenzi.