“Niite bibi Amara!” Kajala ajawa bashasha baada ya bintiye kumfanya kuwa nyanya

Paula na Marioo walimkaribisha duniani binti yao, Princess Amara, Mei 3, 2024.

Muhtasari

•Mpenzi huyo wa zamani wa Harmonize alichapisha video akimkumbatia mjukuu wake na kucheza naye akiwa amekaa kwenye kochi.

•Wakati akitoa tangazo, Paula alimshukuru Mungu kwa zawadi ya mtoto na kueleza jinsi alivyoridhika na kuwa mzazi.

Paula alitangaza kuzaliwa kwa bintiye mnamo Mei 21, hatua iliyomsisimua Kajala.
Image: INSTAGRAM// KAJALA MASANJA

Muigizaji mkongwe wa filamu bongo Fridah Kajala Masanja ndiye nyanya mpya zaidi mjini.

Bintiye Kajala mwenye umri wa miaka 22, Paula Paul alitangaza kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza mnamo Jumanne, Machi 21 na mamake hakuweza kuficha furaha yake.

Mpenzi huyo wa zamani wa staa wa bongo Harmonize alichapisha video akimkumbatia mjukuu wake na kucheza naye akiwa amekaa kwenye kochi.

“Unaweza kuniita bibi amara,” aliandika Kajala chini ya video hiyo aliyoiweka kwenye Instagram.

Paula na Marioo walimkaribisha duniani binti yao, Princess Amara, Mei 3, 2024. Wapenzi hao mashuhuri ambao wamekuwa pamoja kwa takriban mwaka mmoja hata hivyo walisubiri hadi jana Mei 21 kufanya tangazo la mtoto wao wa kwanza pamoja.

Wakati akitoa tangazo hilo, mwanamitindo Paula alimshukuru Mungu kwa zawadi ya mtoto na kueleza jinsi alivyoridhika na kuwa mzazi.

"AMARA❤️ 03/05/2024 Nataka tu kusema Asante Mungu🙏. Moyo wangu umejaa na shukran. Asante kwa kunichagua kuwa mama yako😍 Mungu alijua jinsi moyo wangu unakuhitaji @princess__amarah," alisema Paula.

Kwa upande wake, mzazi mwenza wake Paula, mwimbaji Omary Mwanga almaarufu Marioo alimshukuru Mungu kwa zawadi ya mtoto na kumtakia maisha mema.

“Asante Mungu kwa Baraka hii ya Mtoto , tunakushukuru kwa Mtoto wetu wa Kwanza. Binti yetu mrembo @princess__amarah, Mungu Akukuze akujaalie Afya na Baraka Tele 🙏🏾,” Marioo alisema.

Aliambatanisha kauli yake na video nzuri ya chumba alichojifungua Paula Kajala binti yao.

“ASANTE MALKIA WANGU❤️ @therealpaulahkajala UNASTAHILI KILA KILICHOPO NDANI YA UWEZO WANGU , MUNGU AKUBARIKI SANA,” aliongeza.

Mastaa hao wawili wa bongo walianza kuchumbiana mapema mwaka uliopita, ikiwa ni miezi michache tu baada ya Paula kuachana na mwimbaji Rayvanny ambaye alirudiana na mzazi mwenzake, Fahymah.