Zuchu ajibu kuhusu kumzalia mpenzi wake Diamond

Shinikizo limeendelea kupanda kwa Diamond na Zuchu kufunga ndoa na kuanzisha familia.

Muhtasari

•Mchekeshaji maarufu na mtangazaji wa Clouds Media Mwijaku amekuwa ni mtu wa hivi punde kuchangia suala hilo.

•Tale alimbainishia Diamond kuwa zawadi pekee anayotamani toka kwake mnamo siku hiyo ni harusi yake na Zuchu.

katika ziara yao ya Ufaransa.
Diamond Platnumza na anayedaiwa kuwa mpenziwe, Zuchu katika ziara yao ya Ufaransa.
Image: INSTAGRAM// ZUCHU

Shinikizo limeendelea kupanda kwa wasanii wa Bongo, Diamond Platnumz na Zuchu kufunga ndoa na kuanzisha familia pamoja.

Mchekeshaji maarufu na mtangazaji wa Clouds Media Mwijaku amekuwa ni mtu wa hivi punde kuchangia suala hilo.

"Umzalie MWAMBINO," Mwijaku alimwambia Zuchu chini ya chapisho lake moja kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Chawa huyo wa zamani wa bosi wa Kondegang, Harmonize alikuwa akitoa maoni yake chini ya  chapisho la Zuchu ambapo alikuwa akitangaza shoo yake inayokuja na Diamond inayotarajiwa kufanyika mkesha wa mwaka mpya.

"Je, unakuja? 31/12/2022," aliandika chini ya picha yake aliyochapisha.

Huku akimjibu Mwijaku, binti huyo wa Khadija Kopa alidokeza kuwa atakuwa tayari kumzalia Diamond wakifunga ndoa.

"Awowe," alijibu.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya meneja wa Diamond, Babu Tale kutoa ombi maalum kwa wawili hao kufunga pingu za maisha mnamo siku ya kufunga mwaka huu, Disemba 31,  ambayo pia itakuwa siku ya  kuadhimisha kuzaliwa kwake.

Katika ujumbe wake, Tale alimbainishia Diamond kuwa zawadi pekee anayotamani toka kwake mnamo siku hiyo ni harusi yake na Zuchu.

"Ombilangu kwa ndugu wasanii Diamond Platnumz na Zuchu hii tarehe ni siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwangu, najua kijana wangu Diamond vizawadi vya magari mara nyumba ni sehemu ya kawaida sana kwako ila mimi zawadi pekee utakayo nipa na itakayo ni furahisha siku hii kwanza upige ndoa hata ya watu wanne na mashahidi kadhaa inatosha.

Pili kwenye shoo mkaniimbie kwa pamoja nyimbo yangu pendwa wakati huo mkiwa bibi na bwana harusi kisha tunafunga na kufungua mwaka kwa sura mpya," Tale aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Aliambatanisha ujumbe huo na bango la tamasha ya Diamond na Zuchu iliyoratibiwa kufanyika mnamo Desemba 31.

Tale alithibitisha kuwa yeye kama meneja alitoa idhini ya tamasha hilo litakalofanyika katika Ramada Resort.

"Nilipo pigiwa kuhusu shoo ya tarehe 31/12 tena inafanyika Tanzania nilikua wakwanza kuishawishi ofisi iseme ndio,

Diamond na Zuchu wamekuwa na uhusiano wa karibu mno kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja ambao umepita na kumekuwa na tetesi nyingi kuwa wasanii hao wawili wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi.