Amepigana vita vizuri! CountryBoy aondoka Kondegang.

Muhtasari

• Aliyekuwa msanii katika lebo ya Kondegang, Country Boy ameondoka rasmi katika kundi hilo na kuweka wazi sababu zake za kugura.

• Akizungumza na vyombo vya habari Jumatatu 31/01/2022, Country Boy amesema kwamba anashukuru Harmonize pamoja na usimamizi wa Kondegang kwa ujumla kwa nafasi waliyompa kukuza kipaji chake na pia kuwafikia mashabiki zaidi ndani ya Bongo na ulimwenguni.

Countryboy
Countryboy
Image: Instagram KWA HISANI

Aliyekuwa msanii katika lebo ya Kondegang, Country Boy ameondoka rasmi katika kundi hilo na kuweka wazi sababu zake za kugura.

Akizungumza na vyombo vya habari Jumatatu 31/01/2022, Country Boy amesema kwamba anashukuru Harmonize pamoja na usimamizi wa Kondegang kwa ujumla kwa nafasi waliyompa kukuza kipaji chake na pia kuwafikia mashabiki zaidi ndani ya Bongo na ulimwenguni.

Ameongeza kwamba ni wakati mzuri kwake kuanza safari mpya kama msanii wa kujitegemea na kuwapa nafasi wasanii wengine chipukizi kufanya kazi na lebo hiyo.

Aidha amedokeza kwamba kuna uwezekano wa kuanzisha lebo yake ili kuwasaidia vijana wengi mtaani ambao wanaaminia katika uwezo wake wa kuwashika mkono, na kuwaomba mashabiki kumpa sapoti ili kwa pamoja waweze kuinua vipaji vya Tanzania.

Country Boy pia amegusia swala la utimu ambapo hakuruhusiwa kufanya kolabo na wasanii wa lebo zingine kama WCB, jambo ambalo anakiri liliweza kupunguza kasi ya muziki wake. Amesisitiza kuwa hajawahi kuwa na bifu na msanii yeyote na hivyo yeye yuko radhi kuingia studioni na msanii yeyote atakayekuwa tayari kufanya kazi naye.

Kuhusu ngoma zake ambazo aliziachia akiwa chini ya Kondegang, amewahakikishia masabiki wake kwamba zote zitaendelea kuwa mali yake.

Msanii huyo ambaye amesema kwamba hana chuki yoyote na Harmonize na kuongezea kwamba kwamba ameondoka kwa ihari na wala hajafukuzwa na kwamba gari alilopewa limechukuliwa na usimamizi wa Kondegang.