Kaeni pembeni, hamtajichunguza wenyewe!- Rais Samia Suluhu

• Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu amemuamuru waziri mkuu Kassim Majliwa kusimamia jopo litakalofanya uchunguzi wa mauaji yaliyofanyika Mtwara.

• Akizungumza na wananchi wa Magu Jijini Mwanza Ijumaa tarehe 4/2/2022, Samia Suluhu amesema kwamba kulingana na taarifa zilizomfikia ni kwamba, mauaji hayo yalifanikishwa na jeshi la polisi na hivyo basi hawawezi kujichunguza wenyewe.

Rais Samia Suluhu wa Tanzania
Rais Samia Suluhu wa Tanzania
Image: GOOGLE

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu amemuamuru waziri mkuu Kassim Majliwa kusimamia jopo litakalofanya uchunguzi wa mauaji yaliyofanyika Mtwara.

Akizungumza na wananchi wa Magu Jijini Mwanza Ijumaa tarehe 4/2/2022, Samia Suluhu amesema kwamba kulingana na taarifa zilizomfikia ni kwamba, mauaji hayo yalifanikishwa na jeshi la polisi na hivyo basi hawawezi kujichunguza wenyewe.

Kuna mauaji yametokea Mtwara na kwa taarifa zilizopo ni Jeshi la Polisi ndilo lililofanya mauaji, taarifa nilizonazo jeshi limeunda Kamati kufanya uchunguzi, haiwezekani Jeshi lifanye mauaji halafu lijichunguze lenyewe, nimemuelekeza Waziri Mkuu aunde Kamati nyingine iende ikafanye uchunguzi wa mauaji yaliyofanywa na Polisi, nataka pia Jeshi la Polisi lijitafakari waone kilichotokea ni misingi ya Polisi au vinginevyo,’’ alisema Suluhu.

Mheshimiwa Samia Suluhu ambaye alichukua hatamu za uongozi kutoka kwa hayati John Pombe Magufuli anaonekana kufanya kila juhudi kuhakikisha wananchi walioaminia uongozi wake wanapata haki.

Pia ameliomba jeshi kujitafakari ili kufahamu iwapo misingi yao inajengwa na mambo tatanishi kama hayo ama vinginevyo.

Katika hotuba yake kwa wananchi, mama Samia Suluhu amewaomba wananchi kudumisha amani  na kutojihusisha na visa vyovyote vinavyoweza kuchangia vurugu na kutoa taarifa muhimu kwa polisi ambazo zinaweza kuwatia nguvuni wote wanaovuruga amani ya taifa.

Kwa sasa inasubiriwa kuona utofauti kati ya ripoti iliyowasilishwa na jeshi na ile itakayowasilishwa na jopo linaloongozwa na waziri mkuu Kassim Majaliwa.