Ssaru sio mpenzi wangu - Trio Mio

Muhtasari

• Msanii Trio Mio amekana madai kwamba yupo kwenye mahusiano na mwanamuziki mwenzake, Sylivia SSaru.

• Hii ni baada ya wasanii hao kuonekana wakiwa karibu kwenye video ya ngoma yao mpya.

Trio Mio
Image: Instagram

Msanii Trio Mio amekana madai kwamba yupo kwenye mahusiano na mwanamuziki mwenzake, Sylivia SSaru.

Hii ni baada yao kuachia kibao #KichwaTu na mashabiki wakakisia kuwa wawili hawa wanachumbiana kutokana na jinsi walivyoonekana kuwa na ukaribu katika video ya ngoma hiyo.

Hata hivyo Trio amefutilia mbali kauli hizo akisema kwamba hakuna chochote kinachoendelea kati yao wawili na kwamba ukuribu wao kwenye video ulilenga kujenga mazingira mazuri ya kuachia kazi nzuri itakayowafurahisha mashabiki.

Akizungumza na Mpasho, msanii huyo amesema kwamba Ssaru ni msanii mwenzake tu na kuwaomba mashabiki kukoma kuzua mambo yasiyo ya kweli.

Staa huyo ambaye anaonekana kutasua kwa kasi katika  burudani la Kenya amesema kwamba aliishi kutamani kufanya kazi na Ssaru kwa muda mrefu kwa kile alichokitaja kwamba mwanamuziki huyo ana kipaji kikubwa na kwamba anajituma katika kazi zake.

Ameongeza kwamba anafurahia  hatua alizozipiga licha ya umri wake mdogo, huku akitoa hakikisho kwamba atazidi kuwaburudisha mashabiki kwa kmuziki mzuri.