'Wababa' hawatulii, wanataka kutoka kimapenzi na mimi - Mylee Staicey

Muhtasari

• Mke wa msanii Weezdom, Mylee Staicey amekiri kwamba ‘wababa’ wanamtafuta usiku na mchana wakitaka awe mchumba wao.

• Akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habri nchini, Staicey amesema kwamba wanaume hao wamekuwa wakitoa ahadi za hela nyingi kwake ili kumrai kuingia katika mtego wao wa kimapenzi.

Mylee Staicey
Mylee Staicey
Image: Instagram KWA HISANI

Mke wa msanii Weezdom, Mylee Staicey amekiri kwamba ‘wababa’ wanamtafuta usiku na mchana wakitaka awe mchumba wao.

Akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habri nchini, Staicey amesema kwamba wanaume hao wamekuwa wakitoa ahadi za hela nyingi kwake ili kumrai kuingia katika mtego wao wa kimapenzi.

Aidha ameongeza kwamba siku mbili zilizopita kuna Yule aliyejitolea kumnunulia gari aina ya Range Rover ila hakuitikia mwito huo.

“Kwanza siku mbili zilizopita kuna mmoja alikuwa anataka kuninunulia gari, alisema kwamba niko sawa na akaniambia niende katika sehemu yoyote ya kuuzia magari nichukue itakayonipendeza,” alisema Staicey.

Mylee Staicey ambaye alionekana kubana maneno kwa kuwa mumewe alikuwepo studioni kipindi mahojiano hayo yanafanyika, anakisiwa kukubali ahadi hiyo kutoka kwa ‘mubaba’ akisema kwamba angefurahi kutumia gari hilo katika kampeni .

Mwanadada huyu katika siku za hivi karibuni aliweka wazi kwamba atawania kiti cha ubunge katika eneo la Kibwezi Magharibi.

Mashabiki kwa upande wao wamemwambia kwamba yeye ni mrembo katika ulingo wa siasa lazima atakumbana na visa kama hivyo, basi ajipange ipasavyo.

Kwa sasa kinachosalia kuwa kitendawili ni mumewe, Weezdom alichukuliaje swala hilo na je uhusiano wao utasalia kuwa imara ulivyokuwa?