Mbosso afunguka kuhusu mahusiano yake

Muhtasari

•Msanii huyo wa WCB hata hivyo alikiri kuwa kuna wanawake wengi ambao amepata watoto nao nchini Tanzania.

•Machache tu yanajulikana kuhusu mahusiano ya Mbosso kwani sio kawaida yake kuyaweka wazi wala kuchumbia wanadada mashuhuri 

Image: INSTAGRAM// MBOSSO

Staa wa Bongo Mbwana Yusuf Kilungi almaarufu kama Mbosso ameweka wazi hali yake ya mahusiano ya sasa.

Akizungumza na wanahabari katika tamasha ya Mahaba Ndi Ndi Ndi  iliyoandaliwa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Mbosso alitangaza kwamba kwa sasa hana mchumba yeyote.

Alisema kwa sauti iliyoashiria kwamba hata kama hana mpenzi kwa sasa, huenda yuko katika harakati za kutafuta.

"Mimi niko single, kama una dada nitunuku" Mbosso alisema.

Msanii huyo wa WCB hata hivyo alikiri kuwa kuna wanawake wengi ambao amepata watoto nao nchini Tanzania.

Mbosso alisema hana mahusiano tena na baby mama wake yeyote na kueleza kuwa wengi wao tayari wameolewa kwingine.

"Mababy mama wote wako nyumbani kwao. Wengi wao washaolewa, siwezi anza kuchukua wake za watu" Mbosso alisema baada ya kuulizwa kuhusu waliko wazazi wenzake.

Machache tu yanajulikana kuhusu mahusiano ya Mbosso kwani sio kawaida yake kuyaweka wazi wala kuchumbia wanadada mashuhuri kama ilivyo ada ya wasanii wenzake hasa kutoka Bongo.

Mbosso ni mmoja wa wasanii waliotumbuiza kwenye tamasha ya Mahaba ndi ndi ndi lililofanyika usiku wa wapendanao maalum kwa Zuchu.