Sipati chochote kutoka kwa wimbo "omoyo" - Harmonize

Muhtasari

• Msanii wa bongofleva ameweka wazi kwamba hachukui hata senti moja kutokana na mapato ya wimbo wa ‘omoyo’ alioshirikishwa na mchungaji Jane Misso

Harmonize

Msanii wa bongofleva ameweka wazi kwamba hachukui hata senti moja kutokana na mapato ya wimbo wa ‘omoyo’ alioshirikishwa na mchungaji Jane Misso

Akiandika kwenye Instagram yake, Harmonize amesema kwamba hana umiliki wowote katika wimbo huo licha ya lebo yake ya Konde Gang kutumia gharama nyingi kwenye mradi mzima wa ngoma hizo, ikiwemo sauti na video.

Aidha msanii huyo ameeleza kwamba uamuzi wake wa kutodai chochote kutokana na mapato ya wimbo huo unaozidi kurindima na kuteka anga Afrika Mashariki ni kwa sababu aliona ni vema kuutoa kama zawadi kwa wanawake wote wanaojituma katika mishe zao na kumtegemea Mungu.

“Achilia Mbali Mapenzi Yangu Kwa Huu Wimbo ..!!! Hii Project ni Kama Zawadi Kwa Wakina Mama Wote Duniani ..!!! Hasa Wanao Mtegemea Mungu Taarifa Licha Ya Kusimamia Ghalama za RECORDING AUDIO & VIDEO Sina Umiliki wa Huuu Wimbo Hata Kwa 1% Huuu Wimbo Still Unamilikiwa na Mwenyewe MCHUNGAJI @jane_ebeneza_misso Furaha Yangu Ni Kumuona Mama Akiwa Amerejesha Furaha Yake na Kung'aa Kwa Barakha Za Mungu Na UPENDO WENU USIO NA KIPIMO kwa Mama ..!!!! ENDELEA KUTAZAMA LINK KWENYE BIO YAKE @jane_ebeneza_misso & @kondegang TUKUTANE TABATA SHULE @afroeastcarnival”