H-Baba adokeza kilichomtoa kwa Harmonize, ajiita H-Dangote

Muhtasari

• H-Baba amemsifia Diamond na kusema kwamba atampost kwenye Instagram. pia ametangaza kujiita H-Dangote, ikiwa na maana kwamba anamfagilia Diamond sana ambaye pia anajiita Dangote.

H-Baba
Image: Instagram

Msanii mwenye utata H-Baba amezidi kukoleza utata wake kwenye mitandaoni ya kijamii baada ya kuonekana kuwachonganisha Harmonize na Diamond.

Wikendi iliyopita, msanii huyo kwqa mara ya pili tena chini ya wiki mbili ame unfollow Harmonize baada ya kufanya hivo awali na kisha kumfollow tena na safari hii ana ubuyu kuhusu hatua hiyo.

Msanii huyo katika moja ya post zake Instagram ambapo ameweka video ya msalishaji S2Kizzy akisema kwamba nia yange ni kuona wasanii wanapendana, H-Baba ameupigia debe ujumbe huo ila akamaliza kwa kusema kwamba ugomvi umepitwa na wakati na sasa yeye amebasilisha jina na kujiita H-Dangote.

Image: Instagram

Wiki jana Wasafi TV walipakia sauti ya msanii huyo akihojiwa kwenye YouTube yao na ingawa hakusema wazi kwamba ni Harmonize alikuwa anachimba mikwara lakini mazungumzo yote yalikuwa wazi kwamba mhusika katika gumzo hilo alikuwa ni msanii Harmonize.

Kwenye mahojiano hayo, H-Baba alisema kwamba ame unfollow kila mtu na atakaye kuja kujaa hapo kwenye orodha ya wale anafollow ni Simba, kwa maana ya Diamond Platnumz.

H-Baba alisema kwamba kule aliteseka sana kwa kutumiwa lakini hakuwahi fadhiliwa na safari ya nje ya nchi hata moja.

“Pasipoti haina muhuri hata mmoja mpaka inataka kuexpire kweli jamani. Sijaondoka, sijafanya chochote. Hata Kenya sijaenda jamani,” aliteta H-Baba.

Alipochechewa kwamba haukuwa ungwana yeye kuachwa na badala yake Ibraah kupewa nafasi ya kuenda Marekani, H-Baba anasema kwamba suala hilo lilimdhalilisha mtu mzima na ndevu zake.

“Kweli jamani, mimi na midevu yote, nilidhalilika. Nakuambia sina hamu yoyote kwa yaliyonikuta,” alisema H-Baba kwenye sauti yake hiyo iliyochezwa mubashara kwenye radio ya Wasafi na kupakiwa kwenye YouTube.

Pia alimpigia debe Diamond Platnumz na kusema kwamba yupo juu sana na amemjua tangia zamani Zaidi ya mtu yeyote yule.

“Mimi nasema jamani sikilizeni niwaambie kitu, mimi namjua Nasib (Diamond Platnumz) kuliko mtu yeyote na nishawahi waambia, namjua kuliko mtu yeyote. Kwa hiyo aache kusingizia kwamba natumia sijui nini, muda wako ukishafika, umefika. Huu muda si wa kwake, Simba karudi,” anasema H-Baba katika maongezi ambaayo yanatumia maneno fiche kwa wingi.