H-Baba akana madai ya kugombana na Harmonize, amchana Mwijaku

Muhtasari

• H-Baba amekana madai ya kulipiwa kodi ya nyumba na kusema kwamba hayo ni madai tu ambayo yanasambazwa na Mwijaku, akisema kwamba alilipiwa kodi na Harmonize na baadae kukosana naye

• “Mtu hawezi kujichonganisha na Harmonize, hatuwezi. Mimi Konde Boy ni mwanangu na jana nimempatia tuzo ya albamu bora ya Afro East,” alisema H-Baba katika mahojiano na Clouds Media.

H-Baba
Image: INSTAGRAM

Msanii mwenye utata ambaye amekuwa akizungumziwa sana mitandaoni kuhusu utata wa kupakia picha za Diamond na Harmonize kwenye ukurasa wake wa Instagram na kufollow Diamond na ku unfollow Rafiki yake wa karibu, Harmonize, amesema ni simu yake ilizama majini.

Msanii huyo ambaye alisema kwamba picha hizo za wasanii hao wawili ambao hawaonani jicho kwa jicho zilijipakia kwenye ukurasa wake kwa sababu simu yake ilizama majini.

Madai yalivuma mitandaoni kwamba urafiki wao umevunjika na msanii Harmonize, haswa baada yak u unfollow msanii huyo ila yeye ameweka wazi kwamba Konde Boy ni Rafiki yake na hata juzi amempa zawadi ya albamu bora ya Afro East.

“Mtu hawezi kujichonganisha na Harmonize, hatuwezi. Mimi Konde Boy ni mwanangu na jana nimempatia tuzo ya albamu bora ya Afro East,” alisema H-Baba katika mahojiano na Clouds Media.

Msanii huyo pia amepuuzilia mbali madai kwamba amewahi lipiwa kodi ya nyumba na kusema kwamba hizo ni porojo tu

“Mimi naishi Mwanza na ni mfanyabiashara na nimejijengea misingi mizuri ambayo inanifanya nisigonge hodi na hiyo sio tabia yetu Wasukuma kuomba. Mimi ni mtoto wa pekee kwetu hivyo lazima nipambane kwa ajili ya familia yangu na umaarufu wangu ninao toka nikiwa na miaka sita nashangaa sana kuona mtu ananyanyuka na kuniongelea ilihali hanijui hata kidogo kwamba nimeomba hela ya kodi nikapewa million mbili sasa hiyo million mbili naweza kupata nyumba mjini ila nabaki namuangalia tu” alisema H-Baba

H-Baba amesema kwamba Mwijaku alijaribu tu kuwagonganisha na Harmonize na akasisitiza kwamba hajaingia popote wala hajatoka popote baina ya Konde Gang na WCB Wasafi.

“Mimi sijawahi jitoa sehemu yoyote, na pia sijaenda sehemu yoyote. Ndugu yangu yule (Mwijaku) anatakiwa atulie na atuache mimi na Harmonize tumetoka mbali. Wakati tunapambana vita yetu sisi wawili yeye hakuwepo. Kwa hiyo ndugu Mwijaku kuwa makini sana,” alisema H-Baba katika mahojiano hayo