H-baba aomba msamaha baada ya kuposti video ya Diamond

Muhtasari

• Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, H-baba  ameomba mashabiki wake msamaha baada ya kupakia video ya Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram

• H-baba amechapisha ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram akiomba watu wa hisani wamsaidie kununua simu nzuri.

H-baba
H-baba
Image: Hisani

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, H-baba  ameomba mashabiki wake msamaha baada ya kupakia video ya Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram.

H-baba amechapisha ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram akiomba watu wahisani wamsaidie kununua simu nzuri.

"Samahani ndugu zangu hii imejiposti yenyewe sijui kuna nini, hii  simu nilionayo sielewi mwenye ushabiki wa kweli  na mimi aninunulie simu napata taabu kuposti na hii simu," alisema H-baba.

Kauli imewadia baada ya H-baba kumsifia Diamond Platnumz kualikwa kwenye tamasha za Grammy kutumbuiza.

Licha ya H-Baba kuwa na urafiki mkubwa  na msanii  Harmonize, mambo yameonekana kuwa yanachukua mkondo mwningine siku za hivi majuzi ambapo msanii huyo ameonekana akimpongeza Diamond.

Alieleza kuwa simu aliyokuwa anatumia hapo awali ilianguka majini na kwa sasa hana simu ya kuwasiliana na marafiki zake.

simu  yangu ilianguka kwenye maji na nimeanika juani, sijui itakuwa sawa lini bado nasubiri, kwa sasa sitakuwa hewani mpaka nitakapo pata simu," alieleza