H-Baba azidi kuchanganya mashabiki zaidi

Muhtasari

• Msanii mkongwe wa ngoma za bongo fleva amezidi kuzua maoni kinzani baada ya kupakia picha za Diamond na Harmonize mara tofauti.

• Haya yanqakuja siku chahce baada ya ku unfollow Harmonize na ku follow Diamond ambaye ni adui wa kimuziki wa Harmonize

Harmonize, H-Baba na Diamond
Image: Facebook

Msanii mkongwe wa ngoma za bongo fleva amezidi kuzua maoni kinzani ya kutatanisha mno kwa siku za hivi karibuni huku akionekana guu moja Kondegang na guu la pili WCB Wasafi

Post zake nyingi za wiki jana kwenye ukurasa wake wa instagram zilikuwa ni kuhusu msanii Diamond Platnumz huku akidai kwamba ni hongera alikuwa anammiminia kwa kuwa mwanamuziki wa kwanza kutoka Afrika mashariki kutumbuiza kwenye tamasha la Grammy Global Spin

H-Baba ambaye amekuwa na uswahiba wa karibu na msanii Harmonize alizua madai mapya baada ya ku unfollow Harmonize na ku follow Diamond Platnumz, huku wengi wakisema kwamba huenda amevunja mikataba yake na msanii Harmonize ambaye siku za hivi karibuni hawaonani jicho kwa jicho na aliyekuwa bosi wake Diamond Platnumz.

Madai hayo hata yalichochewa zaidi pale ambapo msanii Harmonize alitoa bango la orodha ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha lake la Afro East Carnival mnamo mwezi Machi ambapo kwenye orodha hyo jina la H-Baba lilikosekana kabisa.

Februari 13, H-Baba amepakia video ya kutangaza tamasha hilo la Harmonize, ambapo amezidi kuwachanganya wengi wa wafuasi wake wasijue ni nini kinaendelea katika kichwa cha msanii huyu.

Katika video hiyo, H-Baba ameambatanisha ujumbe wa kuwataka watu wote kuelekea kwenye tamasha hilo.

"Mwanza...!!!! We go Crazy 26/2/ ROAD TO @afroeastcarnival Tabata Shule 5/3/ 🐘 @the_cask_bar_grill POWERD BY @jembefmtz" aliandika H-Baba.

Mbali na hilo H-Baba pia amebadili profile picture kutoka ya Diamond Platnumz ile aliyoiweka siku chache nyuma na kuweka picha ya Harmonize

Je, unahisi H-Baba anajaribu kukileza uhasama kati ya Diamond na Harmonize ama ndio anajaribu kuwapatanisha?