Mbosso aibua hisia tofauti mitandaoni baada ya kukiri anataka kuwa 'single' milele

Muhtasari
  • Yeye ni baba lakini hayuko kwenye uhusiano na baby mama wake
  • Hata hivyo ameingia kwenye mitandao yake ya kijamii kuandika taarifa ambayo haijawapendeza mashabiki wake wengi

Mbosso ni mwimbaji maarufu kutoka Tanzania ambaye pia amesajiliwa chini ya lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platinumz.

Mbosso anafahamika kuachia nyimbo nzuri sana ambazo nyingi huwa ni za mapenzi ambazo wanandoa wengi wanaweza kuzihusisha nazo.

Mashabiki wamekuwa wakiuliza mwanamke mwenye bahati anaweza kuwa nani maishani mwake Ili amwimbie huku akionyesha upendo wake.

Yeye ni baba lakini hayuko kwenye uhusiano na baby mama wake.

Hata hivyo ameingia kwenye mitandao yake ya kijamii kuandika taarifa ambayo haijawapendeza mashabiki wake wengi.

Ambayo ujumbe ulionyesha kuwa ana mpango wa kubaki single milele.

Aliandika " single forever ."

Ni nini kingeweza kumfanya afanye uamuzi kama huo, inaweza kuwa kuvunjwa roho kutoka kwa mahusiano ya zamani?

Ni ujumbe ambao uliibua hisia mitandaoni, na hizi hapa baadhi ya hisia zao;

iamlavalava: Unadanga Mbwa Wewe @mbosso_ 😂

platnum36_2O: oow mshedade sikuizi unaunyamafran I iviii wa Chibu🔥🔥 ,nakukubarisaana #wcb4life

baefeelings_tz: Kama uko single usiangalie status zangu 🙌🙌🙌

pamuku_boy13: Au sio kijana muhuni sana😂😂

officialgeor_tz: Single!? Wakat mama chanja yupo maeneo umemtuliza😂