Mbosso atinga streams milioni 60 Boomplay.

Muhtasari

• Msanii wa WCB, Mbosso Khan afikisha streams milioni 60 katika mtandao wa Boomplay.

• Kupitia ujumbe ambao ameachia katika ukurasa wake wa Instagram, Mbosso amejiita ‘’king’ kwa hatua hiyo aliyoipiga kuhakikisha muziki wake umewafikia mashabiki wengi ndani ya Bongo na ulimwenguni kote.

66855938_1220357588125307_5681176959875639446_n
66855938_1220357588125307_5681176959875639446_n

Msanii wa WCB, Mbosso Khan afikisha streams milioni 60 katika mtandao wa Boomplay.

Kupitia ujumbe ambao ameachia katika ukurasa wake wa Instagram, Mbosso amejiita ‘’king’ kwa hatua hiyo aliyoipiga kuhakikisha muziki wake umewafikia mashabiki wengi ndani ya Bongo na ulimwenguni kote.

Diamond Platinumz ambaye ni bosi wake, amempongeza kwa hatua hiyo ambayo ameitimiza katika safari yake ya muziki.

Mashabiki pia hawajaachwa nyuma baada yao kujitokeza kwa wingi kumpa kongole Mbosso kwa bidii ambayo ametia katika mchakato wa kuhakikisha anatoa kazi za kufurahisha.

Ngoma ya hivi punde kutoka kwa msanii huyo ni #ForYourLove ambayo alimshirikisha msanii mwenzake katika lebo hiyo ya WCB, Zuchu.