Hatimaye Mulamwah aanza ujenzi wa nyumba yake kijijini kwao

Muhtasari

• Hatimayemcheshi Mulamwah ameanza ujenzi wa nyumba yake kijijini mwao, kaunti ya Trans Nzoia.

• Kupitia video aliyopakia katika ukurasa wake wa Instagram, mcheshi huyo alionyesha lori likimwaga changarawe katika sehemu ambayo kujenga.

Mulamwah
Image: Facebook
Mulamwah
Image: Facebook

Hatimayemcheshi Mulamwah ameanza ujenzi wa nyumba yake kijijini mwao, kaunti ya Trans Nzoia.

Kupitia video aliyopakia katika ukurasa wake wa Instagram, mcheshi huyo alionyesha lori likimwaga changarawe katika sehemu ambayo anatarajiwa kujenga.

Mulamwah alimshukuru Mungu kwa hatua hiyo, huku akiwarai vijana wenzake kuzidi kupambana kwani ipo siku ndoto zao zitatimia.

“Mungu ni mkuu, tunazidi kupiga hatua. Vijana msipoteze mwelekeo, yote yanawezekana,” Mulamwah aliandika.

Hatua hii inajiri siku chache tu baada ya kutengana na aliyekuwa mpenzi wake, Carol Sonnie ambaye alisema kwamba alikuwa anataka maisha ambayo yalikuwa nje ya uwezo wa Mulamwah.

Kwa siku kadhaa mcheshi huyo alionekana akipakia picha katika mtandao wa Instagram akiwa ameshikilia hela nyingi na kusema kwamba angetaka kujenga nyumba yake huko kijijini.

Awali pia Mulamwah alizungumzia kuhusu umuhimu wa kujenga na kutengeneza mazingira mazuri kijijini ili mambo yakikwenda vyongo mjini unapata sehemu ya kukimbilia.

Mulamwah ni moja kati ya wacheshi wachanga ambao wamepiga hatua kubwa kimaisha, huku akizidi kutoa tumaini kwa chipukizi wengi ambao wangependa kufuata nyayo zake.