Trio Mio afikisha 'streams' milioni moja kwenye Boomplay

Muhtasari

• Ngoma zote za Trio Mio kwenye jukwaa la Boomplay zimefikisha 'streams' milioni moja kwendqa mbele.

Image: INSTAGRAM// TRIO MIO

Msanii wa kizazi kipya ambaye ni mchanga Zaidi kuwahi kutokea katika kazazi hiki nchini Kenya Trio Mio amefikisha ‘Streams’ milioni moja kza ngoma zake zote tangu aanze kuimba na kuzitundika kwenye jukwaa la kusambaza miziki la Boomplay nchini Kenya.

Trio Mio ambaye ngoma zake zilipokelewa vizuri kabisa na Wakenya bado ni mwanafunzi wa shule ya upili lakini badi anakaza buti kwenye tasnia ya muziki huku hivi karibuni akifichua siri yake ya kusawazisha masomo na muziki kwa usanjari alisema kwamba aliamua kuhamisha masomo yake nyumbani ili iwe rahisi kwake kufanya vyote viwili kwa mkupuo.

Msanii huyo pia aliwashangaza wengi aliposema kwamba mama yake ndiye meneja wa muziki zake na wakati mwingine humsaidia kutunga mashairi yake.

Nguli huyo wa ‘cheza kama wewe’ ni miongoni mwa wasanii wa gengetone ambao wanatamba sana nchini huku kila msanii akimng’ang’ania kufanya collabo na yeye, ya hivi karibuni na ambayo inatesa ni ‘Sipangwingwi’ ambayo mpaka imeanza kutumiwa katika baadhi ya hafla za kisiasa, haswa na naibu rais William Ruto.

hivi majuzi kulikuwa na kadi ya kulipiza kwenye hafla mbalimbali ya msanii hiyo, kadi ambayo ilikuwa inaonesha msanii huyo akisema anadai shilingi elfu kumi za Kenya ili kuonekana katika mahojiano na vyombo vya habari.

Unapenda ngoma yani ya Trio Mio?