Diamond anakiri Rayvanny ndiye mwenye riziki kubwa Wasafi

Muhtasari

• Diamond alisema Rayvanny ana heshima mno pamoja na kwamba ana ukichaa wake na anashika nafasi ya pili kwa kuingiza kipato baada yake.

Diamond, Rayvanny
Diamond, Rayvanny
Image: Maktaba

Msanii na mkurugenzi mkuu wa kampuni nyingi tu chini ya mwavuli wa Wasafi, Diamond Platnumz amekiri kwamba msanii Harmonize nduye aliyekuwa na riziki kubwa sana enzi zake akiwa kwenye rekodi lebo ya Wasafi ila pia akafurahia kwamba sasa hivi amepata mtu ambaye ameziba mwanya huo ifaavyo na kumtaja mtu huyo kuwa ni Rayvanny ambaye alisema kwa sasa ndiye anayepata riziki kubwa sana kutokana na kazi zake za muziki chini ya lebo ya WCB Wasafi.

Diamond alisema kuwa, pamoja na maneno mengi yanayosemwa juu ya Rayvanny kuondoka kwenye lebo hiyo, lakini msanii huyo ana heshima mno pamoja na kwamba ana ukichaa wake na anashika nafasi ya pili kwa kuingiza kipato baada yake.

“Kuna kitu watu hawakijui kuhusu Rayvanny, ana heshima sana, sijui kwa sababu ya kusoma au kuwa giniaz darasani. Lakini kuna kitu ambacho watu hawakijui, Rayvanny anashika nafasi ya pili kwa kuingiza pesa ndani ya Wasafi,” alisema Diamond akiendelea kupromoti EP yake ya First Of All (FOA).

Kumekuwa na minong’ono mingi tu kwamba msanii Rayvanny baada ya kuanzisha lebo yake ya Next Level Music anataka kuigura Wasafi na ambapo wengine wanahoji kwamba kitendo chake yeye kukubali ubalozi wa kampuni ya kubashiri ya PM Bet ambaye ni mpinzani mkuu wa Wasafi Bet yake Diamond ni mojawapo ya ishara kwamba anataka kuiasi Wasafi na kuwa msanii huru.

Lakini mkubwa wake Diamond Platnumz amelikanusha hilo na kusema kwamba next Level Music ni kama mtoto wa Wasafi na wawili hao hawatenganishiw kwa gharama yoyote ile.