Pesa ni kila kitu, naweza nikanunua binadamu yeyote - KRG

Muhtasari

• Msanii na mfanyibiashara KRG the Don amesema kwamba anachukia umaskini na watu wanaoabudi umaskini.

• "... ukiwa na pesa hata unaweza kujipeleka hospitali," KRG alisema.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: KRG the Don

Msanii na mfanyibiashara KRG the Don amesema kwamba anachukia umaskini na watu wanaoabudi umaskini.

Mwanamuziki huyo alisema kwamba pesa ndo kitu cha pili binadamu wanapaswa kutafuta baada ya Mungu.

Akizungumza katika mahojiano na mwanablogu Kesh Gracy, KRG alisema kwamba pesa inasaidia kusuluhisha matatizo mengi na kumsaidia mtu kuishi maisha mazuri.

Alisema kwamba mtu akiwa na hela anaweza kununua mtu yeyote na kufanya chochote anachotaka.

"... ukiwa na pesa hata unaweza kujipeleka hospitali," KRG alisema.

KRG alishikilia kwamba kila jambo analolifanya katika maisha yake lazima liwe la kuleta hela, na kwamba hathamini urafiki ambao unamrudisha nyuma kimaendeleo.

Aidha, alisema kwamba hataki kupendwa na kila mtu, kwani yeye anapambana kukimbiza ndoto zake binafsi.

Madai haya yanajiri siku chache baada ya kushuhudiwa vurugu baina yake na wasanii wa kundi la Mbogigenje, ambao walimwambia kwamba kuwa na hela sio kila kitu katika maisha ya binadamu.