Mimi sio size yako, Mungai Eve amkaba Andrew Kibe

Muhtasari

Mungai Eve amemsuta Andrew Kibe kwa kuingilia maisha yake.

Amesema kwamba anapaswa kujiheshimu kutokana na umri wake mkubwa.

instagram KWA HISANI
instagram KWA HISANI
Image: mungai eve

Mwanablogu Mungai Eve amemtupia cheche kali aliyekuwa mtangazaji Andrew Kibe cheche kali kwa kile alichokitaja kama kuingilia masuala ya maisha yake binafsi.

Akizungumza katika mahojiano na Presenter Ali, Mungai alisema kwa muda sasa Kibe amekuwa akimkosea heshima kwa kujihusisha na mahusiano yake na mpenziwe Trevor.

Mungai alikiri kwamba hampendi kwa tabia yake ya kuhisi kwamba anajua kila kitu na wanaume katika jamii wanapaswa kufuata ushauri nwake.

"Mimi simpendi, sitaki mambo yake, sijui mbona anahisi anajua watu wanapaswa kufuata ushauri wake," Mungai alisema.

Aidha alisema kwamba Kibe ni mtu anayejutia kutotumia ujana wake vizuri na sasa ana chuki akiona vijana kama yeye wakitengeza hela nyingi na kuishi maisha mazuri kuliko yake.

Alimtaka atafute pesa kwa utulivu bila kuingilia maisha ya watu, huku akishikilia kwamba hamuogopi hata chembe.

"Yeye mwenyewe alipewa talaka na anataka kuwashauri watu kuhusu ndoa, anapaswa kuingia katika kuhubiri labda," aliongezea.

Mungai Eve ni moja kati ya wanablogu ambao wanajituma sana katika kazi zao na kuzidi kutoa tumaini kwa chipukizi wengi kwamba kila kitu kinaweza kutoa kukiwa na bidii.