Erick Omodi amnunulia 'mpenzi' wake gari katika birthday yake

Muhtasari

• Mcheshi Omondi amemnunulia 'mpenzi' wake gari katika siku yake ya kuzaliwa.

• Alisema ni zawadi ndogo ya kumpongeza kwa bidii yake.

Mcheshi Erick Omondi amewashangaza mashabiki baada ya kumnunulia 'mpenzi' wake gari katika siku yake ya kuzaliwa.

Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Omondi alisema kwamba gari hilo lilikuwa zawadi ndogo kwa Lynne kutokana na bidii yake katika mishe zake.

"Nimemnunulia Lynne zawadi ndogo ya siku yake ya kuzaliwa. Napenda bidii yake na najua ataenda mbali," Omondi alisema.

Mashabiki hawakuachwa nyuma huku wakijitokeza kwenye 'comment section'  kumpongeza Omondi kwa hatua hiyo na kumtakia Lynne heri katika siku yake ya kuzaliwa.

Aidha kuna wale walimtupia cheche wakisema kwamba penzi lao halitadumu kwa muda mrefu.

"Mtaachana tu," shabiki mmoja aliandika.