Mbona wasanii wanatafuta kiki? Mashabiki wanasemaje?

Muhtasari

• Katika siku za hivi karibuni wasanii wengi wameonekana kutafuta kiki ili kusukuma muziki wao.

• Mashabiki kwa upade wao wamekuwa a kauli kinzani kuhusu mtindo.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Bahati, Vivianne na Willy Paul

Muziki ni kipengele muhimu katika jamii kwa kuwa unafunza na kuburudisha watu.

Wasanii kwa upande wao hutumia mbinu mbalimbali kuhakikisha wanazalisha muziki mzuri utakaodumu na kupendwa na mashabiki.

Kwa muda sasa katika taifa la Kenya, asilimia kubwa ya wasanii wamelalamika kwa kile walichokitaja kuwa mashabiki wanasherehekea sana wanamuziki wa mataifa ya nje na vyombo vya habari kucheza miziki ya nchi za nje.

Hali hii imewapelekea wasanii wengi kulazimika kutumia mbinu mbadala ili kazi zao na wao wenyewe kukubalika.

Sio siri kwamba kiki imekuwa mbinu moja ambayo imetumika na wasanii kusukuma kazi zao, huku kukiwa na mjadala mkubwa kuhusu madhara yake miongoni mwa mashabiki na washikadau mbalimbali wa burudani.

Mara kwa mara kuna wasanii ambao wamefanya kiki kali ila muziki wao ukatokea kutokuwa na mashiko. Je wasanii wanatumia hela na akili nyingi na kusahau kwamba wanapaswa kuwekeza sana katika muziki?

Kuna wale pia ambao wamepata ufanisi mkubwa kupitia kiki hizi na hata kujipatia hela nyingi baada ya kuachia miziki yao.

Baadhi ya wasanii ambao wamefanya kiki ni: Bahati, Willy Paul, Weezdom, huku wa hivi karibuni wakiwa Vivianne na Sosuun.

Sio siri kwamba kuna wasanii ambao viwango vyao vya kimuziki vilishuka baada ya kuanza kujihusisha katika kutafuta kiki.

Licha ya kwamba kiki huzua hisia moto miongoni mwa mashabiki, inawadia muda ambapo wanachoka na hata kuacha kusapoti wasanii hao kwa kile kinachosemekana kuwa kiki zinawafanya wapoteze hadhi zao.

Huko Tanzania kiki ni jambo la kawaida, huku mashabiki wakiwa wameshazoea mazingira hayo kabla wanamuziki waachie kibao.

Itakuwa haki zaidi kusema kwamba kiki zinakata kote kuwili; zinajenga na kubomoa wasanii.

Je wewe kama shabiki ama mshikadau wa burudani una lipi la kusema kuhusu kiki katika muziki?