"Mkosi jamani!" Alikiba akemea ndoto ya kuoa mwanamke mweusi

Muhtasari

• Msanii Alikiba amewashangaza wengi baada ya kuitra mkosi, ndoto iliyomjia ya kuoa mwanamke mweusi.

• Alikiba aliikemea ndoto hiyo na kuwataka mashabiki wake kumuombea pia.

Alikiba
Alikiba
Image: Instagram

Mwishoni mwa wiki iliyopita, msanii Alikiba aliwashangaza wengi baada ya kudai kwamba anahitaji maombi kutoka kwa mashabiki na wafuasi wake walokole kwa sababu ya kuota kuwa ameoa mwanamke mweusi.

Katika kile kilichotafsiriwa kwamba msanii huyo hapendi wanawake Weusi, aliandika kwenye Instagram yake akisema kwamba ameota akifunga pingu za maisha na mwanamke mweusi na kukemea ndoto hiyo vikali.

“Mkosi jamani nahitaji maombi yenu leo nimeota tena naoa mwanamke mweusi TOKA PEPO,” alikemea Alikiba.

Kulingana na maneno yake hayo aliyoyaandika kwenye instastories zake, inaashiria kwamba huenda si mara ya kwamba anapata ndoto kama hiyo kwani alisisitiza kwamba ameiota tena.

Miezi michache iliyopita, msanii huyo aligonga vichwa vya habari baada ya vununu kusambaa kwamba mkewe alikuwa katika mchakato wa kuelekea mahakama ya Kadhi jijini Mombasa ili kutalikiana na Alikiba, kwa kile baadhi walihisi kwamba ni kutokana na mwanamke aliyeonekana akicheza densi kimahaba na msanii huyo kwenye video ya ngoma yake ya #Utu.

Juzi alipoulizwa kuhusu Sakata la kuachana na mkewe, Alikiba aliwafokea wanahabari kwa kucharuka kwamba ni mke wake na kuwataka wakome kufuatilia mambo ya ndoa za watu, jambo ambalo lilionekana kumgusa mfupa wa ndani.