Diamond: Sitaki kuoa! Kuoa kutanizuia kutoa muziki mzuri, nimeliona hili kwa rafiki zangu

Msanii huyo alisema kuoa labda akishastaafu kutoka kuimba muziki

Muhtasari

• Alisema kwamba hana mpango wa kuoa kwa sababu anataka kuzidi kuachia madude mazito ya muziki.

• Ila pia hakupuuzilia mbali suala hio kwani alidokeza kwamba pengine huenda akaoa wakati amekaribia kustaafu muziki.

Msanii Diamond Platnumz
Msanii Diamond Platnumz
Image: Instagram///Diamond Platnumz

Msanii Diamond Platnumz amesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba hana mpango wa kuoa na kutulia kwenye ndoa muda wowote hivi karibuni kwani kulingana na yeye bado anataka kufanya muziki sana.

Akizungumza katika mahojiano ya moja kwa moja wakati wa ziara yake nchini Ujerumani, Diamond aliulizwa ni lini anapanga kutulia kweney ndoa ikizingatiwa kwamba umri nao unazidi kuzikwenda kwa kasi mno.

“Unapanga lini kutulia lini, yaani lini unaoa mwanamke?” Diamond aliulizwa.

“Una maanisha nini, mimi tayari nimeshatulia. Lakini hiyo unajua mimi bado nataka kuwapa muziki kwa sana, mimi chenye nimeona ni kwamba nikioa mwanamke basi atanitoa kwenye njia yangu ya kufanay muziki na kuvuruga azma yangu ya kufanay muziki, nimeliona hilo kutoka kwa rafiki zangu wote. Kwa sasa wacha niwape muziki na ikifika muda nimekaribia kustaafu basi nitaoa,” Diamond alisema.

Alipoulizwa muda kamili wa kufanya hivo, msanii huyo alionekana kukwepa kabisa na kusema kwamba muda wowote tu hivi karibuni chochote kinawezekana na kusisitiza kwamba hawezi kupanga vitu bali ni Mungu ndiye mpangaji wa vyote.

Kwa muda mrefu Diamond amekuwa akihusishwa na kuwa katika mahusiano na msanii wa kike kwenye lebo yake ya Wasafi baada ya kuachana na wapenzi wake wa awali akiwemo Mkenya Tanasha Donna, Muganda Zari Hassan na Mtanzania Hamisa Mobetto ambao wote kila mmoja amemzalia Diamond mtoto, Zari akiwa na wawili wa Diamond.

Aidha msanii huyo alikanusha dhana kwamba anawachezea wanawake na kisha kuwaacha baada ya kuwazalisha watoto. alisema kwamab heshima yake kwa watu wote wenye jinsia ya kike ni ya juu sana na kuwataka wanawake wote kutokubali wanaume wawachukulie poa na kuwachezea kaam hawataki wenyewe.