Inachukiza! Hamisa Mobetto awapa onyo kali wanaume wanaomtumia picha za uchi

Pia amewaonya wanaume wanaojaribu kumtongoza kwa kutuma kila aina ya jumbe za uchochezi.

Muhtasari

•Mama huyo wa watoto wawili ameonekana kukerwa na tabia hiyo na kuwataka wahusika kukoma mara moja.

•Pia amewaonya wanaume wanaojaribu kumtongoza kwenye mitandao ya kijamii kwa kutuma kila aina ya jumbe za uchochezi.

Image: INSTAGRAM// HAMISA MOBETTO

Malkia wa Bongo Hamisa Mobetto amejitokeza kuwakashifu wanaume wenye tabia potofu ambao wamekuwa wakimtumia picha za uchi wao.

Mama huyo wa watoto wawili ameonekana kukerwa na tabia hiyo na kuwataka wahusika kukoma mara moja.

"Tafadhali acheni kunitumia picha za uchi wenu. Inachukiza na inakera!!" Mobetto alisema kupitia ukurasa wake.

Alidokeza kwamba amekuwa akiwablock wafuasi wenye tabia kama zile, jambo ambalo amelichoka kabisa sasa.

"Nimechoka sana kuwablock washenzi" Aliandika.

Mzazi huyo mwenza wa Diamond Platnumz pia aliwapa onyo wanaume ambao wamekuwa wakijaribu kumtongoza kwenye mitandao ya kijamii kwa kutuma kila aina ya jumbe za uchochezi.

Alifichua jumbe za jamaa mmoja aliyejaribu kumtongoza kwa kudai katuma shilingi milioni mbili za Tanzania kwa ajili yake.

"Mnikome na hizi meseji zenu za aina hii. Nini mbaya na wengine wenu?!" Alisema Mobetto.

Kwa kipindi mrefu mwanamitindo huyo amekuwa akijaribu kuficha hali yake ya sasa kuhusu mahusiano.

Takriban miezi miwili iliyopita hata hivyo, rapa wa Marekani Rick Ross alithibitisha tetesi ambazo zimekuwepo kwa muda kuwa wanachumbiana.

"Wanataka kujua kama tunachumbiana," Hamisa alimwambia Rick Ross kupitia mazungumzo ya moja kwa moja kwenye Instagram na akajibu, "Ndiyo ni wangu".

Hamisa hata huvyo amekuwa akiwanganya mashabiki kuhusu suala la kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na rapa huyo.

Katika mahojiano ya awali alidai kuwa uhusiano wake na Rick Ross ni wa kirafiki tu na haijawahi kutokea zaidi ya hicho.

"Hakujawahi kuwa na mahusiano. Huwa ananipa makopakopa kwa sababu nafanya naye kazi. Hakuna chochote. Pindi kikitokea kama kuna kitu mtafahamu," Mobetto alisema mwezi Mei katika mahojiano na Clouds Media.

Msanii huyo amewahi kuwa kwenye mahusiano kadhaa na kutoka. Tayari ana watoto wawili ambao alipata na wapenzi wawili wa zamani, Francis Majizzo na Diamond Platnumz.