(+video) Njugush asimulia aibu baada ya mwanamke mnene kumkumbatia na kuanguka na yeye

Alijitetea kwa kusema kwamba alianguka na huyo mwanamke kwa sababu kipindi hicho hakuwa amekula vizuri

Muhtasari

• "Kuamka kutoka pale chini ilikuwa ni dakika moja kwangu ambayo ilikuwa yenye aibu kubwa,” Njugush alisema.

Muigizaji na mcheshi Njugush
Muigizaji na mcheshi Njugush
Image: Instagram//Njugush

Muigizaji na mcheshi Njugush ambaye kipindi cha nyuma alikuwac anaonekana kioja kutokana na umbile lake la wembamba uliopitiliza amezungumza kitu ambacho amewahi pitia cha kuabisha mno katika maisha yake.

Katika video ambayo ilipakiwa kwenye mitandao ya kijamii na wakiza maudhui, walikuwa wanamuuliza mjasiriamali huyo maswali ya kiutani tu ambapo katika hilo alielezea kwamab alikuwa mjini kipindi hicho bado alikuwa na wembamba na mama mmoja mnene ambaye alisema ni shabiki wake alimkimbilia na kumkumbatia na wote wawili wakapukutika chini kama majani ya mti.

“Ilikuwa ni mama mmoja ambaye ni shabiki wangu ni mkubwa kiumbile, sasa alikuja mbio akanikumbatia tukaanguka na yeye. Kipindi hicho sikuwa nimekula vizuri. Kuamka kutoka pale chini ilikuwa ni dakika moja kwangu ambayo ilikuwa yenye aibu kubwa,” Njugush alisema.

Mchekeshaji huyo pia alichukua nafasi hiyo kuzungumzia sekta ya Sanaa nchini na kusema kwamba ina nafasi kubwa sana kwa kila mtu mwenye talanta kutokana na kile alisema kwamba ukiangalia ushuru ule ambao unatokana na mapato ya wasanii wa aina zote nchini inakuonesha wazi kwamba kitivo hicho kina nafasi kubwa sana ya kuwakuza watu wengi wenye vipaji.

Aidha, akizungumzia kitu ambacho alimfanyia mke wake na kikamfurahisha pakubwa, Njugushi alisema kwamba hawezi sahau kipindi ambapo alimpikia ugali uliochanganyishwa na viazi na karoti na kusema kwamba hicho ndicho chakula kitamu zaidi ambacho mke wake anakisifia kutoka kwake mpaka leo hii.

Msanii huyo amekuwa akielezea vitu vingi vya maisha yake na familia katika kipindi chake cha Through Thick & Thin ambacho anakipakia kwenye wavuti wake kila mwaka, na alisema kwamba wakati anaanza kuigiza hakuwa anafikiria angefika kule ambako amefika wakati huu.